Marehemu Arafa Hamisi Billal
( 1962- 2011) enzi za uhai wake


Jumuiya ya Watanzania Italy kwa masikitikiko makubwa imepokea taarifa za msiba wa Shangazi yake Dada Sophia ambaye anaishi Castel Volturno CE -Italia Marehemu ARAFA HAMISI BILAL amefariki siku ya jumapili nchini India ambako alikuwa huko kwa matibabu. Mipango ya mazishi inafanywa ambapo mazishi yatafanyika siku ya jumatano kwenye makaburi ya kisutu jijini Dar Es Salaam.

Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Italia kwa niaba ya Watanzania wote waishio Italia inaungana na wazazi,ndugu,jamaa na wafanyakazi wa Uwanja wa ndege wa kimataiafa wa MWALIMU NYERERE ambako marehemu alikuwa akifanya kazi,katika kuomboleza na kuwaombea MwenyeziMungu awape uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba.


Mola aiweke roho ya Marehemu mahala pema peponi
-AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Poleni sana wafiwa huyu dada alikuwa mchangamfu na kwenye kauli nzuri kila wakati, mara nyingi nilikutana naye pale airport dar.
    Namkumbuka akifanya kazi pale Airport pamoja na shaima(mbunge viti maalum)wote walikuwa wacheshi na ulipokuwa na tatizo hawakusita kukusaida.Mziko saa ngapi wengi tugependa kuhudhuria kwani alikuwa mtu wa watu.
    INNA LILAHI

    ReplyDelete
  2. Mungu amlaze mahala pema peponi Amina mfanyakazi mwenzetu Amina.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...