Kaimu mkuu wa Mkoa Mbeya Moses Chitama akiwatuliza wananchi wenye jazba ya kusimamishwa mganga wa jadi Jafari Willina kutoa tiba ya ukimwi na magonjwa mengine sugu baada ya kutulia kaimu mkuu wa mkoa huyo aliwaeleza wananchi kuwa serikali ya mkoa imeruhusu kuendelea kupata kikombe hicho cha dawa kwa kuzingatia taratibu zote za afya pia na kumuagiza kijana Jafari kutafuta eneo jingine kubwa lenye maji na choo kwani hapo alipo sasa si eneo salama sana kwa afya ya binadamu.
Jafari willina akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuruhusiwa kuendelea kutoa dozi ya kikombe kwa tiba ya magonjwa sugu.
Kaimu mkuu wa mkoa Moses chitama na kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa mbeya Advocate Nyombi wakimsikiliza mmoja wa wagonjwa Hassan akitoa ushuhuda wa dawa ya Jafari.
Mzee Anangisye naye hakuwa mbali na kuandamana kupinga kusitishwa kwa kikombe cha mabatini

Picha na Mbeya Yetu Libeneke dada la Globu ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. dah!hii sasa kali, kwani kila kukicha anaibuka nabii mpya mwenye kikombe.ila swali moja najiuliza ,kwani hao manabii ni wanaume tu? huyu mungu anaubaguzi au ? oh1 sorry nilisahau yule mwanamke wa tabora,anyway kama mungu ameamua kutupendelea watanzania vile, ni mtizamo 2

    ReplyDelete
  2. ...the hopeless society of Tanzanians...trully we are back 200 years compared na wenzetu...

    ReplyDelete
  3. Mangi wa KiboshoMarch 29, 2011

    Ipo siku mwendawazimu atasema 'ameoteshwa' kuchanganya mavi ya binadamu na maji iwe dawa ya UKIMWI na watu watajaa kupata kikombe

    ReplyDelete
  4. i dont reaaly blame them kama serikali imeruhusu why not. pesa ya haraka haraka hapo. tuitakula wapi?

    ReplyDelete
  5. hii inaonyesha jinsi serikali imeshindwa kuwapa wananchi huduma bora za hospitali. Watu wanakimbilia kwenye hivi vikombe viwe salama au si salama. Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  6. Headache

    ReplyDelete
  7. na mimi uncle na dawa yangu sitozi shilingiiiii.! ila mimi sio nabiii.

    ReplyDelete
  8. Hivi! Hawa watu wanaoibuka sasa hivi na tiba ya vikombe wakikuwa wapi siku zote? Hii inadhiirisha wazi kuwa wanaiga tu kwa sababu kwa nini wanatumia vikombe kama babu loli??? Aah! Huu ni upumbavu.

    ReplyDelete
  9. hii sasa wanataka kuanza mambo ya udini kwa vile aligundua dawa mkirsto na sasa mwiislam wanataka kupima kama serikali itawakataza waanze mambo yao ya udini tuombe mungu atusaidie na kulijua hili maana sisi binadamu ni vigumu kuelewa hizi ni nyakati za mwisho majaribu ni mengi sana

    ReplyDelete
  10. I call it,
    THE JOHN MASHAKA epidemic!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...