Kumekuwa na wasiwasi mkubwa kwa Watanzania walio na ndugu, jamaa na marafiki nchini Japani juu ya usalama wao unaotokana na kutokea kwa majanga makubwa ya tetemeko la ardhi na Tsunami.
Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani (Tanzanite Society) kwa kushirikiana na mtandao wa Watanzania wanaoishi nchini Japani (wanatija), pamoja na ofisi zetu za ubalozi hapa Japani tunapenda kuchukua fursa kuwataarifu kuwa mpaka sasa tumeweza kuthibitisha kuwa karibu watanzania wote wako salama.
Taarifa hii inamaanisha kuwa hatujapata taarifa zozote za Watanzania walioathirika na janga hili mpaka sasa zaidi ya uharibifu wa mali kutokana na tetemeko na tsunami. Tumeweza kuthibitisha kuwa watanzania walioko Fukushima na Sendai (maeneo yaliothirika zaidi) wote wako salama.
Tutaendelea kutoa taarifa kwa kadri tutakapokuwa tunapata habari mpya. Kwa wale ambao wangependa kupata taarifa za ndungu zao tafadhali wasiliana nasi kwa kutumia anuani:
chairman@tanzanitesociety.jp.
Utakapotuandikia tafadhali tupe taarifa zifutazo kama unazifahamu: Jina kamili, mji anaoishi na namba yake ya simu au anunai yake. Unaweza pia kutupa namba yako ili tuweze kukutaarifu kwa haraka.
Ahsanteni.
Uongozi.
Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani.
Soma Taarifa kutoka Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Japan.
kumbe hawa jamaa hawana nyumba wala nini wanaishi kwenye makaratasi tu
ReplyDeleteMchangiaji wa kwanza!Unajua ni kwanini wanajenga hizo nyumba unazoziita za makaratasi au unaandika tu "makaratasi". Inaonyesha teknolojia mzee iko mbali na milango yako. Pole sana utaendelea kubahatisha maisha hapo bongo, au popote ulipo wakati wenzako wanafikiria jinsi ya kuendelea.......
ReplyDeleteMtoa maoni hapo juu, umenifurahisha sana.Ni Kweli nyumba zao nyingi ni za karatasi kwa sababu wanajua majanga yanavyowapata kila mara. ndugu zetu ni kuwaonea huruma na kuwaombea kila siku, Japan nchi ya Kimbunga, Volcano, tetemeko, Mafuriko. Shukuru Mungu aliwapa utajiri mwingi. Nchi kama zetu Bongo tungekuwa tumesha wote kabisa. Baada ya miezi mitatu tu nchi ya Japan itarudi kwenye hali yake ya kawaida.
ReplyDeleteplease namtafuta rafiki angu juma kapuya yuko japan na familia yake kama kuna yeyote an habari zake naomba tafadhali
ReplyDeleteJapan kuna Juma Kipaya na siyo Kapuya,kama ni Kipaya yupo salama pamoja na familia yake,na yeye ndiye mtunza hazina mkuu wa jumuia ya watanzania Japan.
ReplyDeletemdau Japan.
mimi naamini mungu anatupenda. umefika kipindi watu tumuelekee. Naamini majanga kama haya hayatokei ila pale watu wanapomsahau muummba, na dhulma kuenea. najuwa kutakuwa watu watakaosema mimi nazungumza pumba lakini Maneno haya nayaandika kwa kuangalia maafa yaliyopita duniani. na kama unayeamini dini yeyote basi wimbo ni mmoja.
ReplyDelete