Ankal na ndugu wadau wapendwa,

Kunua wizi mpya umeingia Dar es salaam na inawezekana ukasambaa hata kwenye miji mingine mikubwa. Wizi huo uko hivi:

1. Unaweza kupewa kipeperushi ambacho kimepuliziwa dawa na baada ya kupokea aliyekupatia ambaye anajifanya anauza bidhaa anazozitangaza kwenye kipeperushi hicho anakufwatilia kwa nyuma na gari nyingine na kukupora kila kizu baada ya wewe kupoteza fahamu.

AU


2. Ukiwa unaendesha gari vijana wanakufwata na kukushitua kuwa gari inawaka moto then utafungua dirisha kutaka kuona nap engine kusimama. Watakwambia hakuna kitu vijana wanakudanganya hao. Ndani ya muda huo mfupi kwa namna ya ajabu ukifungua tu dirisha wanakupulizia madawa yenye radha na harufu kama pipi tamuu na kukufwatilia kwa matumaini kwamba utapoteza fahamu na wao kukunyanganya mali zako including kupora baadhi ya vitu kwenye gari.

HIVYO KUWENI MAKINI UNAPOENDESHA GARI USIFUNGUE VIOO WALA KUPOKEA KIPEPERUSHI AU KUNUNUA NUNUA HOVYO CHOCHOTE KWENYE HIZO FOLENI ZA DAR . PIA WANAFANYA HUO UCHAKACHUZI WA FAHAMU HASA MAENEO YA PETROL STATION NA MAENEO YA MAEGESHO YA
MAGARI KAMA MLIMANI CITY.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Sasa Kaka Misupu,

    Tusifungue vioo vya magari na joto lote hili la Daresalamu? Mweeh!

    Wengine tuna VIMEO havina a/c wala feni.

    Itakuwaje?

    ReplyDelete
  2. Itabidi mtebee na max ukipewa kipeperushi kabla ya kufunguwa uvae max.

    ReplyDelete
  3. Duuh hii ni Balaa ikifika Bushi kwetu huku si ndio tutalia mpaka tukomee...Asante kwa hii Nuziii

    ReplyDelete
  4. Pambaf!! wajinga ndio waliwao!

    ReplyDelete
  5. haya ni maisha gani??Dar kila siku wizi na utapeli,watu wengi wamejazana hapo hawana kazi,wanataka starehe na utajiri wa haraka haraka bila kutoa jasho !!"mishen town"sijui hali hii itaisha lini?Ukienda mikoa au baadhi ya wilaya fulaani utaona population ni ndogo sana,watu wote wamejazana hapo Dar,ndiyo maana kila siku uhalifu,mauaji,ufuska nk.haviishi,haijulikani ichukuliwe hatua gani ili kuweza kukomesha vitendo vya kihalifu ??
    mkulima Kisarawe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...