Wafanyakazi wa Exim wakishusha misaada Gongo la Mboto
Wakitoa misaada ya nguo na chini wakiitembelea
moja ya familia zilizoathirika


WAFANYAKAZI wa Benki ya Exim wametoa vyakula na mahitaji mengine mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya Sh. mil 5.1/= kwa waathirika wa mlipuko wa mabomu eneo la Gongo la Mboto, Dar es Salaam.

Vitu vilivyotolewa na wafanyakazi hao ni pamoja na sare za shule kwa wanafunzi mbalimbali walioathirika, unga wa Sembe, Mchele, Unga wa Ngano, Mafuta ya Kula ,Sukari, Chumvi,Maharagwe, Sabuni na Majani ya Chai.

Meneja Masoko Msaidizi Anita Goshashy alikabidhi vitu hivyo kwa niaba ya wafanya kazi wenzake kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecki Sadiki ambapo alitoa rai kwa wafanyakazi wengine kama wao pamoja na wadau mbalimbali kuendelea kujitokeza kusaidia wahanga husika.

Alisema msaada huo ni katika kuthamini utu wa watanzani wenzao waliopatwa na mkasa huo ambao kwa namna moja au nyingine ni nguvu kazi ya taifa hivyo wanapaswa kufarijiwa kwa kuwapa msaada.

“Tumesikitika na kuguswa kwa namna ya kipekee na tukio lililowapata wenzetu nasi kama miongoni mwa wadau tunatoa msaada wetu wa vyakula na vitu vingine na wale waliojeruhiwa tunawaombea wapone haraka,”alisema

Kwa upande wake Mkuu huyo aliishukuru benki hiyo na kuiomba kuongeza tena msaada mwingine kama uwezo utawaruhusu kwani mahitaji bado ni mengi.
“Tunawashukuru kwa jinsi mlivyoguswa na kuamua kujitolea kwa kiasi mlichoweza,lakini bado tunatoa rai kwenu na kwa wadau wengine kujitolea zaidi endapo uwezo unawaruhusu kufanya hivyo kwani mahitaji bado ni mengi”, alisema mkuu huyo.

Benki hii pamoja na msaada huo,imeshatoa mchango wa damu kwa waathirika husika mapema wiki iliyopita ambapo pia hatua hiyo ililenga kuchangia benki ya damu katika hospitali ya Taifa Muhimbili inayohudumia majeruhi wengi zaidi wa majanga mbalimbali yanayotokea nchini .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...