Kaka Ankal,
Katika pita pita zangu, nimekutana nah ii nyumbani ambayo inajengwa kama mita 150 hivi toka nyumbani kwa Diwani wa kata ya Kijichi. Eneo moja linalojulikana kama kwa Mabenz (fundi pekee wa Benz kijichi).

Basi bwana, kama picha inavyojieleza, jamaa anajengea ndani ya nyumba yake zile nyaya ambazo husapoti nguzo isianguke sasa sijui kama akimaliza kujenga atautoa waya au utabaki kuwa sehemu ya nyumba yake.

Kaaazi kweli kweli...
TANESCO mpooooo?

Kama wakitaka niwalelekeze, wakujuze utanichek niwaelekeze. Maana huu ni uvunjifu wa sheria na hii ni sehem tu ya uvunjifu unaofanyawa na wananchi. Tatizo la mashirika yetu kazi nyingi hufanyika ofisini. Kwa maoni yangu huku tunakoelekea ni pabaya. Iko siku utakuja kukuta nguzo iko sebuleni next time.

Mdau Sele

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Acha unoko wewe wivu tu mwenzako anajenga banda lake la kukujisitiri we unaanza uzandiki

    ReplyDelete
  2. GEORGE GELAIMarch 14, 2011

    ACHA WIVU WEWE KWA KUWA HUNA NYUMBA NDICHO KINAKUUMA JENGA YAKO BWANA ACHA ROHO MBAYA JAMAA ANAJENGA KIWANJANI KWAKE ILA TANESCO WAMEVAMIA KUWEKA NGUZO KIWANJANI KWA JAMAA SIYO JAMAA KENDA KUJENGA KIWANJANI KWA TANESCO ELEWA HIVYO NA TANESCO NDIYO WANAOTAKIWA KUONDOA NGUZO YAO PALE KIWANJANI KWA JAMAA JUWA HILO.

    ReplyDelete
  3. mwacheni hivyo hivyo Tanesco wakitoa nguzo si tutakosa umeme jamani.nchi ishaposwa hii kila mtu ajifanyie atakavyo...ila nnavyoona itabidi aukate huo waya(stay)

    ReplyDelete
  4. Hapana ukweli lazima usemwe kwani kama huna nyumba ndo useme ukweli??

    Ninyi wachangiaji hapo juu ndiyo miongoni mwa waafrika waliyo zoea kuishi kwa mazoea bla kufuata taratibu.

    Je, nguzo hiyo ikishika moto hayo mnayosema mtayasema tena????

    ReplyDelete
  5. Mbona hii ni kawaida hapa kwetu bongo, nakumbuka wakati jamaa wanajenga bara bara ya kinyerezi kutoka pale relini kuelekea kinyerezi mita kama 100 hivi kulikuwa na nguzo ndani ya barabara ilibidi jamaa waendelee na ujenzi kwa kuacha nguzo pale ndani ya barabara, watu tulizoea kuikwepa hiyo nguzo na mambo kuendelea, baada ya miaka kadhaa wakarekebisha kidogo kwa kusogeza nje ile nguzo. Hivyo wacha jamaa ajenge kajumba kake ipo siku tanesco wataitoa nguzo yao.

    ReplyDelete
  6. huyu jamaa huo muda wa kupiga picha na kija kuirusha hapa,yaonyesha ni wivu..Kesho jamaa wa hiyo nyumba utamuona anaendesha BMW utaanza kuwa ni mwizi na jambazi..wacha hizo bwana..kama imekukera Tanesco unapafahamu, pia kuna ofisi za kijiji nenda basi katoe taarifa hapo..Je unajua kuwa jamaa ameshafanya mipango na Tanesco wahamishe hiyo nguzo..unalitambua hilo..Bongo tambarare..

    ReplyDelete
  7. Before hamja-mbeza mtoa mada someni risk ya kuwa na nguzo hapo ama angalieni uozo huo "no matter nani kaanza na nani kamaliza".

    Kuwa na nyumba si tija ila haitakiwi na haieleweki kuwa hivyo na hivyo tuondokane na akili ya kuamini wivu ama majungu bali angalia ukweli then toeni michango ya kuboresha nchi na sio taarabu zetu.

    Haitakiwi kuwa hivyo period!
    Hatari kwa watoto, raia nk na ni poorest plan kwa mtoa kiwanja na TANESCO nk

    ReplyDelete
  8. Nyie watu nadhani hamuishi uswazi kwanza huyo mjengaji mwenywewe anajenga nyumba au anapanga matofali? nyumba haijengwi hapo bwana
    ukiikagua hiyo nyumba utaona tu ni zilezile za nyumba vyumba sita watu ishirini ndani choo kimoja bafu cjui acheni kushabikia ushamba kwanza kamaliza kiwanja chote sasa garden anadhani ataweka wapi? huko ni kuukaribisha umasikini tu

    ReplyDelete
  9. Mwacheni mwenzenu apate banda lake,halafu mtu amguse wakati Waziri Mkuu ameshasema bomoa bomoa IKOME.

    ReplyDelete
  10. UNAJUWA HAPA KUNA MAMBO MAWILI TUSIOJUWA TUSIPENDE KUDAKIA...

    1. HUYU ALIYEPIGA PICHA KAMA KAONA KUNA MAKOSA ANGEONGEA NA MWENYE NYUMBA INAWEZEKANA KWELI ANA CHUKI BINAFSI ILa...

    2. KAMA KWELI HUYU JAMAA KAJENGA KIHOLELA ANAJIWEKA KWENYE MATATIZO NA HUO UMEME.

    3. KWA MAONI YANGU NAVYOONA HAPO KWA HIYO FENSI YA MCHONGOMA INAONESHA LABDA NI SEHEMU YA JAMAA MSTIMU AMEJENGA NDANI YA KIWANJA CHAKE ISIVYOTAKIWA MWENYE NYUMBA BASI ANA KILA HAKI NA TANESCO WATOWE HUO MSTIMU. KK

    ReplyDelete
  11. Hotmail.comMarch 14, 2011

    Dah! Kaaaaaazi kweli kweli. Yaani mada yenyewe na ukijumlisha na watoa maoni ni kaaaaaaaaazi kweli kweli. Lakini nadhani wahusika wameipata meseji. Ufumbuzi wa mchanganyo huu utatolewa. Ahsante kwa "Mtoa Mada" hii.

    It's Great To Be Black=Blackmannen

    ReplyDelete
  12. We mshamba mwenye wivu wa ajabu. kawanza angalia majiranizake wamejenga vipi. Inaonesha wazi kuwa engineer aliye calculate nguze wanaziweka vipi alikua kalewa gongo. Na wewe utakua unakaa maeneo hayohayo sema jamaa unamchukia tu. Tumekustukia fala wewe.

    Mdau Finland.

    ReplyDelete
  13. Watanzania tunapenda kutumia neno wivu na hili ndilo linaliirudisha nyuma hii nchi.Kama wananchi tutakuwa na msimamo mmoja na tukaijali hii nchi basi na hakika kila mtanzania ataifuata sheria.Kwani haya mambo ya kiholela ndio yanaleta madhara pamoja na kukaribisha rushwa ndani yake.Nimeshaona vioja vingi tu mtu anauziwa kiwanja ikiwa ni sehemu ya barabara sasa hapo jamani tutafika kweli na haya maendeleo tunayoyataka?Halafu tunawapigia viongozi makelele wakati wakishatuona hatuna msimamo ndio tena nawao wanatumia muda huo kurahisisha mambo yao.Amkeni jamani hebu tufuate mifano ya wenzetu ktk nchi zao.

    ReplyDelete
  14. kaazi kweli kweli kama mtu anajenga kiholela mtu akikosoa eti wivu tutafika kweli hivi.Africa bado kazi tunayo nchi za wenzetu wanaendelea mana wananchi wenyewe wanafwata utaratibu hakuna mambo yakienyeji
    sasa sisi waafrica tunapenda sana mambo ya kienyeji alafu tunailalamikia serikali

    ReplyDelete
  15. Mnaonyeshwa ukweli mnasema wivu. Ndio maana hatutaendelea milele. Angalia google earth mji wetu ...kama kuku kaparua parua yaani utaona aibu. Ukiangalia miji mingine africa inaelewaka lakini wa kwetu ni himmbaya kwa ajili ya nyie mnaojidai wivu wivu. Hiyo ni nyumba nayo ya kuonea wivu jamani au hamjaona nyumba nie? Hiyo ni tatizo na kama yako mengi ni bora kuyapoint out...Ni heri kuondoa moja moja mpaka yashe kuliko kukaa kutwa kusema wivu wivu wakati ni hatari kwa jamii na tukiacha hivi kesho na kesho kutwa itakua balaa...Who are we gonna blame?


    Tumwombe Mungu ampe Babu wa Loliondo na dawa ya kufungua maubongo yetu kwa vile yameganda...Tukielezwa ukweli tunsema wivu....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...