Salam aleikum Kaka Michuzi,
shukran kwa kazi nzuri unayoifanyia Globu ya jamii na watanzania wote kwa jumla.
Kaka,kuna mchezo wa kufana sana uitwayo Rugby ila umewekwa kwenye limbi la sahau huku watani wetu wa jadi(*read Kenya) wakiendelea kubobea na kuiletea nchi yao sifa.
Tanzania kidogo tupo nyuma ya majirani wetu wote hadi kusini,ukilinganisha timu zaidi ya 200 za watani wetu(*read Kenya) na zetu hapa zisizozidi 6(sita).
Kwa maana hii ndio timu za kitanzania zikiwemo Dar leopards,Arusha rhinos,Dar Mambaz, Kili Cats na chuo cha Dodoma zinatia bidii kuiboresha mchezo nchini. Tunawakaribisha uma na yeyote anayeupenda mchezo kujitokeza kusudi tuinue mchezo wetu na mwishoe tuwe na timu timam inayoweza kushindana kwenye ulingo wa kiafrika na dunia.
Mchezo huu una maarufu na ufuatiliwaji mkubwa duniani na ni mojawapo ya namna ya kuitangaza nchi vizuri. ila hatuwezi fikia huko bila kunzia chini na ndicho tunachokifanya sasa kaka Michuzi.
Tunaomba msaada wako kuwahamasisha wenzetu waje tucheze wakiitacho 'the hooligan's game played by gentlemen'.
Kesho jumamosi Arusha wanasafiri huku Dar kujaribu kutupa kichapo,nasi tunawaomba wenzetu wa Dar(mashabiki) waje kushangilia mchezo kule uwanjani TPDC Mikocheni A saa kumi unusu.
Ankal,tunaomba support yako kuwezesha mchezo huu wa kipekee.
Siku njema Kaka Michuzi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...