HITMA ya kuwaombea wanamuziki 13 waliokuwa wa kundi la Five Stars Modern Taarab ambao walipoteza maisha katika ajali ya gari Machi 21 mkoani Morogoro, itafanyika Aprili 17 kwenye ukumbi wa PTA, Temeke.

Katibu wa kamati ya Hitma, Bw. Said Mdoe alisema kuwa shughuli hiyo imepangwa kuanza saa 7.00 mchana na maandalizi yake yanaendelea.

Mdoe alisema kuwa wadau wote wa sanaa na burudani wanakaribishwa katika kisomo hicho pamoja na kuchangia michango yao.

Alisema kuwa michango yako iwasilishwe moja kwa moja kwa mweka hazina (Ashraf Ahmed: 0713232747), au kwa Mwenyekiti (Abbas Mtemvu), Makamu mwenyekiti (Sheikh Omar Alhadi naibu imam wa msikiti wa Kichangani) au Katibu (Said Mdoe, 0713 606109) na utapatiwa stakabadhi.

Pia michango hiyo inawezwa kupelekwa ofisini kwake, Kampuni ya Screen Masters iliyopo Kinondoni mtaa wa Togo.

Wajumbe wengine wa kamati ni m

Mhe. Idd Azan (Mbunge wa Kinondoni), Mhe. Azan Zungu (Mbunge wa Ilala), Mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarab Mzee Yusuf, Naibu mkurugenzi wa TOT Khadija Kopa, Asha Baraka (Mkurugenzi wa Twanga Pepeta), Hadija Shaibu “Dida” kutoka Times FM na Sakina Lioka (Clouds TV) na Mariam Migomba

wa TBC.

Wajumbe wengine ni pamoja na wakurugenzi wa Five Stars Modern Taarab Hamis Slim, Ali J na Feruz Juma, Mkurugengenzi wa Clouds FM Ruge Mutahaba, Abdallah Feresh (Mkurugenzi Dar Modern Taarab).

Alisema kuwa kwa watu wa mikoani wanaweza wakatuma michango yao kupitia M-Pesa kwa namba 0765 111135.

Mwisho…

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nilitoa Maoni kwamba waganga wamekubaliana wajitokeze kwa wingi na vikombe vyao ili Mchungaji aonekane ni mganga tu kama wao ili kumvurugia kwani alishaharibu soko lao.

    Cha kushangaza ni kwamba watu wanamshambulia Mchungajieti dawa yake haiponyi lakini wao (waganga)wakitaka kuuza dawa zao wanasema "DAWA YANGU NI KAMA YA LOLIONDO"

    Watanzania acheni wivu na unafiki. La mwisho nimesikitishwa sana na matamko ya maaskofu wa kipentekoste kutoa matamshi ya kushambulia Mchungaji mstaafu hali ikiwa uongozi wa KKKT umebariki dawa hii.

    Hii ni wazi kuwa wapentekoste wamezoea ugomvi kwani huko kwao hakuna amani kila kukicha ni kutukanana maredioni na kwenye vyombo vya habari.

    Sisi tunamwachia Mungu, na tunaendelea kunywa dawa yetu bila ugomvi. Ugomvi wao tunawaachia wao mabingwa wa malumbano

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...