AC Milan wakichekwa kwa mara ya kwanza baada ya miaka saba

Kaka si mbaya na sisi wadau wa AC Milan tukijiachia kwenye blog yetu ya Jamii..ni ubingwa tulikuwa umenyang'anywa tokea miaka saba iliyopita.

ROME: Timu ya mpira wa miguu ya AC MILAN jana ilifanikiwa kuunyakua ubingwa wa Italia baada ya miaka 7. AC Milan ambayo ilikuwa inaitaji kupata point moja tu kwenye mechi tatu zilizobakia ilitoa droo ya 0-0 na timu ya Roma na hivyo kuinyakua point moja ambayo iliwafanya washangilie ubingwa huu wa Italia. Itakumbukwa kuwa timu ya AC Milan kwenye kipindi cha usajili wa wachezaji walinunua wachazaji machachali kama vile Ibrahimovic, Robihno, Boeteng, Cassano, Van Bommel na Emmanuelson ambao walichangia kwa kiasi kikubwa kuiongezea timu hii ukali.

Baada ya mechi hii, Mmiliki wa timu Silvio Berlusconi amewaaidi mashabiki na kocha kuwapatia zawadi kubwa ya wachezaji mashuhuri duniani ambao hakuwasema lakini dalili zipo kuwanunua wachezaji kama vile Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, Bale wa Tottenham au Essien. Yetu macho tukae mkao wa kula tusubilie kipindi cha ununuzi utakapo anza.

WADAU WA AC MILAN MPO!?

MDAU TOKA ROMA a.k.a Pappino!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 08, 2011

    AC MILAN OYEEE!!! TUPO PAMOJA NAMUONA MZEE GATTUSA KAJAA KAMA GUNIA LA MCHELE!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 08, 2011

    AC MILAN OYEEEEEEEEEEE SAFI SANA IBRAHIMOVIC OYEEE ROBINHO......

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...