Baadhi ya Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na wanachama wao wakielekea katika kituo cha kuanzia maandamano yao ya amani kuelekea viwanja vya luanda nzovwe jijini Mbeya mchana wa leo.
Wanachama wa CHADEMA wakiwa kwenye maandamano ya amani jijini Mbeya mchana wa leo
Wanachama wengine wa CHADEMA wakiwa na mabango mbali mbali katika maandamano hayo ya Amani
Baadhi ya Magari yaliyo kuwepo katika msafara huo.

Picha zote Mbeya Yetu Blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2011

    Sasa mbona hamjasema haya maandamano yalikuwa yanakusudia jambo gani hasa?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2011

    anony wa kwanza, na mie najiuliza kulikoni mleta habari wetu kutupasha roborobo utafikiri gazeti la alasiri?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2011

    Kukosa kazi za kufanya tu, hivi wenye shughuli muhimu utawaona hapo? Loosers!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2011

    CHADEMA naona imekuwa jadi kuandamana. Wanaanzia kwenye makao makuu ya mikoa halafu wilaya zote then baadaye kata na baadaye vijiji na hatimaye vitongoji vyote na wakati huo mwaka 2015 wa uchaguzi utakuwa umeshafika. The baadaye wanaanza kampeni. Wanajiandaa jinsi wantavyoingia ikulu kwa maandamano!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 06, 2011

    nilitamani kujua dhumuni la maandamano hayo

    ReplyDelete
  6. du hujui nini lengo la maandamano chadema ina fanya uenezi wa chama, kuwashukuru wananchi kwa kukichagua kwa kishindo, na vita ya ufisadi mpaka kieleweke.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 07, 2011

    du hujui nini lengo la maandamano chadema ina fanya uenezi wa chama, kuwashukuru wananchi kwa kukichagua kwa kishindo, na vita ya ufisadi mpaka kieleweke.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 07, 2011

    nyie chadema kwakweli mnapenda fujo. ni nini kuandamana kila siku. kuna watu kutoka nje au ndani ya nchi wana washawishi au vipi. kazi mnayo takiwa kufanya ni kutafuta wanachama kila sehemu ya tanzania na sio kufanya maandamano. wenzenu wana wanachama kila mji na kijiji tanzania. maandamano hayata waletea ushindi uchaguzi ujao.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 07, 2011

    kwakweli tumechoshwa na maandamano ya hao Chadema mie naona hao hawana kazi za kufanya.wanajaribu kutafuta kuingia IKulu kwa nguvu na kujaribu kuua Amani ya nchi yetu

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 07, 2011

    mafisadi ndo wanaocomment mbovu hapo juu. Mmeridhika na vicent vya vikao na wizi wa mali ya umma bila huruma. Mnasema hawana kazi nyie mkishaiba na kununua magari ya bei ya juu na kuandamana kwenye trafic lights hapo mwaona maisha mmeyapatia, wakati majority wanaendelea kuhenyeka. Kaeni kimya kama mmeshashiba hela za wizi. Alaaaaah

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 07, 2011

    CHADEMA wamewaiga CUF wa Zanzibar wameleta fujo mpaka walipoingizwa kwenye serikali wametulia.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 07, 2011

    Tatizo Watanzania wameshazoea siasa za kulala usingizi, ukimalizika uchaguzi hakuna siasa, ukifika wakati wa Kampeini mnaambiwa vyama vyama vya msimu msiwachague, sasa mambo hayo yamepitwa na wakati baada ya uchaguzi siasa mpaka uchaguzi mwingine hamuawaoni kenya, siasa makanisani, msikitini, kwenye makongamano, bungeni, kwenye mazishi ndio mambo yalivyo msishangae

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 07, 2011

    endeleeni tu kuandamana na ikulu mtaisikia tu wala msiwe na wasiwasi

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 07, 2011

    mimi hata hawanidanganyi , wanasiasaaaaa woooote wezi , wakipata madaraka tu hawakujui , mi hamnipati hata nikiwa usingizini, bora hawa walioko sasa madarakani wameshashiba angalau kidogo hawaibi sana, nyie CHADEMA mna njaa zenu mkija mtainyonya nchi mpaka ikakuke ....

    HAMNIPATI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...