Video hii inaonesha matukio muhimu yaliyojiri katika mechi kati ya Simba SC ya Tanzania na Wydad Casablanca ya Morocco walipocheza jana, Mei 28, 2011 kuwania nafasi ya makundi ya nane bora kwa kinyang'anyiro cha klabu bingwa barani Afrika. Timu ya Wydad Casablanca ilishinda kwa jumla ya mabao 3 il hali Simba haikuambulia chochote. From http://www.wavuti.com/
Home
Unlabelled
Highlits za Simba SC vs Wydad Casablanca
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Sasa Rage anasema refa aliwafanyia kitu mbaya, kwa vipi? maana hakuna shuti hata moja la hatari Simba walilopiga kuonyesha wangeshinda bila refa kuwaminya! Watanzania lazima tubadilike sana ndipo tupate mafanikio kwenye midani ya michezo.
ReplyDeleteKwenye football hakuna kubahatisha Rage!!!!!!!!
H ha aha ha ha! Tuliyasema haya kabla hawajakwenda. sasa mkate rufaa tena. maana mnadhani mpira unachezwa midomoni! ha ha ha ha!
ReplyDeletesasa msubiri motema pembe wanakuja!
Refa kaumiza kwenye goli la kwanza. Mchezaji wa simba yuko ameumia kalala yeye kapeta na washambuliaji wa Wc wakawa wamewazidi namba walinzi wa simba. Magoli mengine yale ni uchofu tu wa simba.
ReplyDeleteMtu anajilaza chini eti mpira usimamishwa! Hizo za mchangani huko viwanja vya Makurumla na kwingineko.
ReplyDeleteHalafu simba mnafungwa kwa ushambaushamba wenu mnaingia uwanjani mkifikiria mechi ya zamani ya Zamaleki na pia kumtambia Yanga, eti 'sisi ndiyo timu pekee ya Tanzania iliyo.......' ujinga huo cheza mpira kwa wakati huo walioifunga Zamaleki hawachezi kwa sasa.
Rage bonge la kiongozi bomu! Usainiiiiiiiiiiii usaniiiiii tuuuu.......na anakuwa bilionea! bongo kweli tumia bongo uishi.
sisi watanzania tunaongea sana,kiukweli hatuwezi mpira kabisa,tumekalia majungu mara refa,viongozi wetu wa mpira mbumbumbu,sisi mashabiki mbumbumbu,hatuwezi kupiga hatua kwa kuchonga mdomoni badala ya kuwekeza,mtu hujapiga hata shuti moja unasema umeonewa,ipo siku tutapewa marefa wetu na bado tutafungwa
ReplyDeleteNamuunga mkono Rage. Mpira unachezwa uwanjani, mdomoni na kwenye kudai haki. Timu nyingi za kiarabu zinatumia mchezo mchafu. Sef Blatter mwenyewe anatumia mchezo mchafu kuendelea kuongoza FIFA!
ReplyDeleteRage anawafanya watanzania kama mambumbumbu! eti refa kawaonea. kuna mchezaji wa simba alikuwa kalala chini WC wakaendelea. sasa yeye alitegemea nn?! mara ngapi tumewaona Simba hawana fair play kwa timu pinzani. au ndio yale ya mtenda akitendewa?! mmeshafungwa rudini nyumbani mjipange kupunguza magoli ya Motema pembe au mkijitahidi basi hata mbahatishe Ushindi. Mpira hauna propaganda!
ReplyDeleteINAKUWAJE MABEKI 8 AU 10 WANASHINDWA KUWAZUIA WASHAMBULIAJE 4 AU 5 KROSI ZOTE ZILIZOPIGWA HAWA JAMAA WAMECHEZA KWA VICHWA WAKATI BEKI ZA SIMBA ZIPO TU HII INAONYESHA KIASI GANI TUSIVYOKUWA MAKINI NA UCHEZAJI PAMOJA NA UFUNDISHAJI TENA TUSHUKURU HATUKUPIGWA NANE PONGEZI KASEJA. RAGE SIO KIONGOZI YUPO KWA MASLAHI YAKE PIA HATA SISI WAPENZI WA SOKA SIJUI TUKO VIPI? HUYU KIONGOZI KAHARIBU KOTE ALIKOPITA LAKINI BADO TUNAMPA ULAJI TU. SASA UNATUDANGANYA BILA AIBU KUWA MAREFA MAREFA WAPI WAKATI KILA KITU KINAJIONYEHA? USAJILI WENZENU MAJUU HUKO WANAFANYA KWA KUANGALIA NAFASI NA UMUHIMU ZA KUSAJILI NA SIO KUSAJILI KWA MALUMBANO ETI YANGA KASAJILI FULANI NASISI NGOJA TUSAJILI FULANI HAYA MAMBO YAMEPITWA NA WAKATI KUMBUKENI SIMBA NI TIMU KUBWA SANA. HEBU ANGALIENI HII VIDEO NA MTAELEWA NAZUNGUMZIA NINI HAO WAKINA RAGE IMETOSHA SASA MIAKA NENDA RUDI WAPO TU BILA MAENDELEO YOYOTE NA BADO TUNAWAKUMBATIA TENA HATA BAADA YA KUISHUSHA MORO UNITED TAFUTENI VIONGOZI WAPYA WAENYE MIPANGA ENDELEVU SIO HAWA WAZEE WA MJINI
ReplyDeleteMpira hauchezwa kwa midomo kama alivyotangulia kusema mdau pale kati,mmelilia rufaa mkaipata mpira mmeshindwa kucheza si afadhali mngewaacha TP Mazembe waendelee. Tamaa mbaya.
ReplyDelete