Video hii inaonesha matukio muhimu yaliyojiri katika mechi kati ya Simba SC ya Tanzania na Wydad Casablanca ya Morocco walipocheza jana, Mei 28, 2011 kuwania nafasi ya makundi ya nane bora kwa kinyang'anyiro cha klabu bingwa barani Afrika. Timu ya Wydad Casablanca ilishinda kwa jumla ya mabao 3 il hali Simba haikuambulia chochote. From http://www.wavuti.com/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2011

    Sasa Rage anasema refa aliwafanyia kitu mbaya, kwa vipi? maana hakuna shuti hata moja la hatari Simba walilopiga kuonyesha wangeshinda bila refa kuwaminya! Watanzania lazima tubadilike sana ndipo tupate mafanikio kwenye midani ya michezo.
    Kwenye football hakuna kubahatisha Rage!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. H ha aha ha ha! Tuliyasema haya kabla hawajakwenda. sasa mkate rufaa tena. maana mnadhani mpira unachezwa midomoni! ha ha ha ha!
    sasa msubiri motema pembe wanakuja!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 30, 2011

    Refa kaumiza kwenye goli la kwanza. Mchezaji wa simba yuko ameumia kalala yeye kapeta na washambuliaji wa Wc wakawa wamewazidi namba walinzi wa simba. Magoli mengine yale ni uchofu tu wa simba.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 30, 2011

    Mtu anajilaza chini eti mpira usimamishwa! Hizo za mchangani huko viwanja vya Makurumla na kwingineko.
    Halafu simba mnafungwa kwa ushambaushamba wenu mnaingia uwanjani mkifikiria mechi ya zamani ya Zamaleki na pia kumtambia Yanga, eti 'sisi ndiyo timu pekee ya Tanzania iliyo.......' ujinga huo cheza mpira kwa wakati huo walioifunga Zamaleki hawachezi kwa sasa.

    Rage bonge la kiongozi bomu! Usainiiiiiiiiiiii usaniiiiii tuuuu.......na anakuwa bilionea! bongo kweli tumia bongo uishi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 30, 2011

    sisi watanzania tunaongea sana,kiukweli hatuwezi mpira kabisa,tumekalia majungu mara refa,viongozi wetu wa mpira mbumbumbu,sisi mashabiki mbumbumbu,hatuwezi kupiga hatua kwa kuchonga mdomoni badala ya kuwekeza,mtu hujapiga hata shuti moja unasema umeonewa,ipo siku tutapewa marefa wetu na bado tutafungwa

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 30, 2011

    Namuunga mkono Rage. Mpira unachezwa uwanjani, mdomoni na kwenye kudai haki. Timu nyingi za kiarabu zinatumia mchezo mchafu. Sef Blatter mwenyewe anatumia mchezo mchafu kuendelea kuongoza FIFA!

    ReplyDelete
  7. Rage anawafanya watanzania kama mambumbumbu! eti refa kawaonea. kuna mchezaji wa simba alikuwa kalala chini WC wakaendelea. sasa yeye alitegemea nn?! mara ngapi tumewaona Simba hawana fair play kwa timu pinzani. au ndio yale ya mtenda akitendewa?! mmeshafungwa rudini nyumbani mjipange kupunguza magoli ya Motema pembe au mkijitahidi basi hata mbahatishe Ushindi. Mpira hauna propaganda!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 30, 2011

    INAKUWAJE MABEKI 8 AU 10 WANASHINDWA KUWAZUIA WASHAMBULIAJE 4 AU 5 KROSI ZOTE ZILIZOPIGWA HAWA JAMAA WAMECHEZA KWA VICHWA WAKATI BEKI ZA SIMBA ZIPO TU HII INAONYESHA KIASI GANI TUSIVYOKUWA MAKINI NA UCHEZAJI PAMOJA NA UFUNDISHAJI TENA TUSHUKURU HATUKUPIGWA NANE PONGEZI KASEJA. RAGE SIO KIONGOZI YUPO KWA MASLAHI YAKE PIA HATA SISI WAPENZI WA SOKA SIJUI TUKO VIPI? HUYU KIONGOZI KAHARIBU KOTE ALIKOPITA LAKINI BADO TUNAMPA ULAJI TU. SASA UNATUDANGANYA BILA AIBU KUWA MAREFA MAREFA WAPI WAKATI KILA KITU KINAJIONYEHA? USAJILI WENZENU MAJUU HUKO WANAFANYA KWA KUANGALIA NAFASI NA UMUHIMU ZA KUSAJILI NA SIO KUSAJILI KWA MALUMBANO ETI YANGA KASAJILI FULANI NASISI NGOJA TUSAJILI FULANI HAYA MAMBO YAMEPITWA NA WAKATI KUMBUKENI SIMBA NI TIMU KUBWA SANA. HEBU ANGALIENI HII VIDEO NA MTAELEWA NAZUNGUMZIA NINI HAO WAKINA RAGE IMETOSHA SASA MIAKA NENDA RUDI WAPO TU BILA MAENDELEO YOYOTE NA BADO TUNAWAKUMBATIA TENA HATA BAADA YA KUISHUSHA MORO UNITED TAFUTENI VIONGOZI WAPYA WAENYE MIPANGA ENDELEVU SIO HAWA WAZEE WA MJINI

    ReplyDelete
  9. Mdau AvoldMay 30, 2011

    Mpira hauchezwa kwa midomo kama alivyotangulia kusema mdau pale kati,mmelilia rufaa mkaipata mpira mmeshindwa kucheza si afadhali mngewaacha TP Mazembe waendelee. Tamaa mbaya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...