Mchezaji wa timu ya Mkoa wa Singida (Kindai Shooting Stars), Nassoro Issa (19) amefariki dunia leo saa 9 alasiri akiwa mazoezini kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Mwenge, mjini Singida.

Issa ambaye alikuwa mchezaji wa timu ya Aston Villa ya mjini humo alijisikia vibaya wakati akiwa mazoezini na kumuomba kocha wa Kindai Shooting Stars,Abdallah Msamba apumzike. Kocha huyo alimruhusu akapumzike chini ya mti nje ya uwanja.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida (SIREFA),Hussein Mwamba, Issa ambaye aliuwakilisha mkoa huo kwenye michuano ya Copa Coca Cola mwaka 2009 aliomba apewe maji ya kunywa.

Baada ya kupewa maji, alikunywa na kujipumzisha. Baadaye daktari wa Kindai Shooting Stars alikwenda kumuangalia ili kujua hali yake. Hata hivyo baada ya kujaribu kumuinua aligundua kuwa ameshafariki dunia.

Mwili wa marehemu ulipelekwa hospitali ya mkoa na baadaye nyumbani kwa baba yake mjini humo. Mazishi yalitarajiwa kufanyika leo au kesho.

TFF imepokea kwa masikitiko makubwa msiba huo na kutuma salamu za rambirambi SIREFA, hasa ikizingatiwa kuwa mchezaji huyo alikuwa bado kijana hivyo kuwa na fursa pana ya kutoa mchango katika maendeleo ya mpira wa miguu nchini, hasa kupitia Mkoa wake wa Singida.

Mungu aiweke roho ya marehemu Nassoro Issa mahali pema peponi. Amina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 02, 2011

    Ina lilahi waina ilayhi rajiun.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2011

    kwa uzoefu tu itakua amefariki kwa ugonjwa wa moyo aliozaliwa nao(congenital hypertrophic cardiomyopathy,ni common cause of sudden death of young athletes.ili kukinga vifo kwa vijana wa michezo,inatakiwa kila mtu kuchekiwa kabla hajajiunga na michezo,sasa sijui kama tz tunaufuata huu utaratibu au la...inna lillahi wainna ilayhi rajiuna.watz tusipuuze checking b4 kuanza na michezo au madaktari wasidharau pindi mgonjwa akija akitaka ruhusa ya kuanza na michezo,tusisign bila kumcheki...mungu ibariki tz

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...