Habari za kazi Mzee wa libeneke la Kutuhabarisha yanayojili huko kwetu Tanzania na Duniani kwa ujumla. Mimi naitwa Frank Ndasezeye,ni Mtanzania ambaye nimeondoka takribani miaka 8 huko nyumbani kwetu Tanzania.
Sasa hapa nilipo katika nchi hii, kuna nafasi za kupiga box ambazo ningependa niwashirikishe ndugu zangu wa kitanzania maana ni vizuri tukisaidiana hata kwa jambo dogo na kutengeneza urafiki na undugu,Hapa nilipo wakenya wamekuwa wakivutana wao kwa wao kutoka kwao na kuja kupiga box hapa na Mimi nikaona ni bora nijaribu kuwavuta hata wawili watatu mana huwezi jua hata wao wanaweza nisaidia pia kwa njia moja ama nyingine kwa baadaye.
Sijapenda kutaja nchi niliyopo maana waosha vinywa ni wengi na wengi wapo kwa kukatisha tamaa wenzao tu. Ila kwa atakayekuwa yupo tayari basi awasiliane na mimi ili nimpe maelezo kwa kina zaidi.
Sasa hapa nilipo katika nchi hii, kuna nafasi za kupiga box ambazo ningependa niwashirikishe ndugu zangu wa kitanzania maana ni vizuri tukisaidiana hata kwa jambo dogo na kutengeneza urafiki na undugu,Hapa nilipo wakenya wamekuwa wakivutana wao kwa wao kutoka kwao na kuja kupiga box hapa na Mimi nikaona ni bora nijaribu kuwavuta hata wawili watatu mana huwezi jua hata wao wanaweza nisaidia pia kwa njia moja ama nyingine kwa baadaye.
Sijapenda kutaja nchi niliyopo maana waosha vinywa ni wengi na wengi wapo kwa kukatisha tamaa wenzao tu. Ila kwa atakayekuwa yupo tayari basi awasiliane na mimi ili nimpe maelezo kwa kina zaidi.
Email yangu ni; f.ndasezeye@live.com


KWELI DOGO UNA MOYO KUNA WATU WAPO ULAYA HAWATAKI KUWASAIDIA WATU WENGINE WAENDE ULAYA,HATA WALIOPO ULAYA HAWATAKI KUWAAMBIA WENZAO WALIOKO ULAYA KWA SABABU YA ROHO MBAYA NA WIVU ATAMZIDI KIMAENDELEO.
ReplyDeleteMIMI NAWAONEA HURUMA NDUGU ZETU WALIOKO ULAYA WASIVYOPENDANA,UKIWAONA USO UMECHOKA WANASINZIA SINZIA KWENYE MABUS KWA KUFANYA KAZI USIKU NA MCHANA WANALALA JUMAMOSI NA JUMAPILI SIKU ZINGINE KAZI KAZI!HAWAPEANI KAZI KWA ROHO MBAYA.
ENDELEA NA MOYO HUU DOGO MAANA UMEISHA ONA WAKENYA,WAGHANA, WAANGOLA ,WASOMALI NA WENGINE WALIVYO NA UMOJA
wewe ndio wale wanaofanya biashara ya human trafficking..waje ili wakusaidie na wao watasaidiwa na nani? ndio nyie mnaochukua dada zetu kama wafanyakazi wa ndani kumbe mnawapeleka kwenye madanguro ya ufuska...kama unataka kusaidia wape mtaji wajiendeleze huko huko nyumbani wanaweza wakakusaidia ukirudi baada ya mgongo kukataa kubeba boksi zaidi..
ReplyDeleteinakuaje uko miaka nane ughaibuni na bado unabeba box,lazima kuna ulakii,maana asilimia kubwa ya watu walioko ugaibuni kwa miaka uliokaa wana kazi zao za maana.
ReplyDeleteHakuna viza ya kupiga box. Hakuna kitu watu wanaumoja duniani. Kuna watu wazuri na wabaya. Ughaibuni kuna tatizo la watu kuishi haramu, sasa ndio maana watu wanaimbiana, lakini pia bila umoja fulani huwezi kuishi maana maboma ni ghali sasa ukiwa na marafiki mnaweza kuishi vizuri kwa bei ndogo lakini pia msiwe wengi. Watanzania walioko Greece wanaumoja lakini waliokuwepo UK, USA na sehemu nyengine hawana umoja.
ReplyDeleteHakuna Mtz anayewewza kumsadia Mtz mwenzie ila kuharibiana, labda uwe wa kwanza. Au sema ukweli unachotaka na hii nchi kwa sasa wanacutdown kila eneo na wanawasaidiaga wakwao kwanza si sawa na kwetu wakiona ngozi wanaogopa. Kuna mtu kakamatwa huku niliko ambaye ni Mtz alikuwa analeta wanawake huku na kuwafanyia anachotaka bila idhini yao. Hivyo ndugu zangu iweni makini. Maisha ni magumu everywhere.Au useme nchi ulioko ila wa decide but actually economic situation is bad worldwide.
ReplyDeleteKwa maneno mengine bora Tz unaweza kwenda kuomba chumvi next door, ughaibuni sivyo, shida ni yako tena ukimuomba mtz unakutana nalo. Watz wa ughaibuni hata kazi hawapasiani tena wengine wanajiita wakenya, waganda aibu tupu, tena hawaendi na muda, ni wasengenyaji kuliko. Anyway mnauamuzi muitikie mwito.
Huyo aeleze yupo nchi gani? Maana si kila nchi unafika na kuanza kubeba boksi. Nchi nyingine kazi hiyo ya boksi inathamani sawa na nchi nyingine. Ili kuifanya unatakiwa upate kwanza residence permit au work permit. Huyu inawezekana akawa anachemsha tuuu jamii!
ReplyDeletedaaa mdau mmoja unasema sura zimechoka kuliko za bongo manake bongo kijana wa miaka 25 utasema anamiaka 50, licha watu kupiga box mtu wa majuu ukimuona ni tafauti na home,,home watu wamechoka sn na sura zimekunyaa kwa maisha magumu, kheri ya box la huko kuliko hapa manake angalau huko unajilipa hapa pesa kidogo sn hata kijio chako hukipati, hakuna human right, wizi mtupu balaa tupu.
ReplyDeleteSASA HUYU HATASIMWEELEWI ANASEMA KUNA KAZI SASA NA HIYO VISA ATAPATAJE MAANA KUPATA VISA NDIO KAZI KUBWA NA KWANINI HATAKIKUTAJA HIYO NCHI NAONAHUYU ANATAKA KUFURAHISHA WATU TU HAKUNA LOLOTE HIZO NI POROJO
ReplyDeletehuyu jamaa mwongo huku ulaya maisha magumu sana ukosefu wa ajira umefanya hata wazungu kibao wanabeba box, mimi nimekaa ulaya miaka 10 na nimeishi nchi nyingi lakini kwa sasa mimi siwezi kudanganya kazi hakuna,taarifa ya benki ya dunia na hata mtandaoni angalia unemployment ulaya iko hivi spain 20%, portugal 14% Greese 16%, USA 10%, UK 8%, Sweden 9%, Finland 8%,Italy 8%, France 9% na nchi za ulaya mashariki huko ndo hatari kishenzi hakuna ajira. Mimi hapa napiga box na wazungu kutoka Russia, Spain, Italy, USA , na waaFrica toka Kenya, Nigeria na Ghana. Hali ya maisha ulaya imekuwa ngumu sana wakati huu halafu kwa sasa nchi kibao wameanza kupigia kelele sera za uamiaji yaani immigration policies na ubaguzi umeanza kujitokeza sana kule spain, Italy, portugal na hata Finland tumesikia African immigrants wanapata shida sasa wewe inawezekana ipo nafasi lakini ni bora tafuta wabongo waliyo ulaya siyo mtu aje kutoka bongo ni hatari kwa sasa, kuna watu wanafanya biashara ya human trafficking wanatumia mbinu kama yako wengine wanatumia mbinu hiyo kupata pesa , mimi nawashauri watanzania muwe macho ulaya pagumu sana mimi siwapigi vita ila nawapa ushauri wangu, asiye sikia la mkuu huvunjika guu, mimi lawama nimetua.
ReplyDeleteJamani mtakao wasiliana na huyu mtu muwe makini kwa maana kazi hakuna si- America wala Europe especially kama ataomba pesa kwa kukupa maelezo. Mimi nipo Europe zaidi ya miaka 20, kwa sasa kazi hamna kabisaa, wananchi wao hawana kazi wakupe wewe??? Europe na America kuna-recession uchumi wao umeporomoka watu hawana kazi.
ReplyDeleteKazi Ughaibuni ni nyingi. Watu huku hawataki kufanya kazi. Ukiwa huna kazi unalipwa, nyumba unalipiwa, ukijikwaa unalipwa, ukiibiwa unalipwa, ukifanyiwa uhalifu wowote ule unalipwa. Ukifanya biashara kama haitoki unalipwa. Mtaji unakopeshwa, pia unafundishwa jinsi ya kuwa mjasiriamali. Ukifilisika unasamehewa madeni yako. Ukizaa mtoto unalipwa. Asikudangenyeni mtu. Piga uwa lakini ukifika uhaibuni mambo yako mazuri. Si kila nchi ya ulaya ni ughaibuni. Nchi za ughaibuni ni USA,UK,France, Scandinavia, Holland, Germany, Australia, Austria, Italy, Greece, Spain, Portugal, Ireland, New Zealand na Japan. Ujanja ya kuishi ni kuomba ukimbizi, useme unatoka Somali, Afghanistan, Libya na DRC. Njia nyengine ni kwa wale wenye elimu kama udaktari na fani nyengine ambazo wana watu wachache. Pia kama ni mwekezaji unakubaliwa kuishi.
ReplyDeleteKwanza jina lake tu linaonekana ni wa kutoka Burundi au Rwanda. Au kama mtz basi ni wa kuhamia. Kwa kweli kazi sehemu nyingi hakuna. Ila naungana na aliyetoa mawazo kuwa ukijaribu kitu kama hicho ujiandae lolote linaweza kukupata. Kwa watakaojaribu angalieni mkishaambiwa mtoe pesa hata kama ni kidogo mjue mmeliwa. Wanaigeria ni matapeli sana na wanatapeli watu kwa njia hii. Sasa siku hizi wapo wakenya, wabongo, wanyarwanda, wakongo na wazambia nao wameiga utapeli wa kinaijeria. Anyway, siwakatishi tamaa wanaotaka kujaribu bahati yao. Na kama huyu jamaa ni genuine, basi Mungu ambariki kwa sababu wenye moyo wa namna hiyo ni wachache. Kwanza jiulize hana hata ndugu mmoja ambaye yuko bongo hana kazi mpaka awatangazie wtz wote? take care GUYZ!
ReplyDeleteWatanzania mlioko Australia mbona hamsikiki? Nimesikia kuna watanzania wapatao 300 Australia lakini hatujawahi kusikia mna umoja au mnaitana hata kubadilishana mawazo. Kulikon? Tungependa tujue kuna watanzania wangapi wanapiga box majuu. Huenda tukaungana tukaleta mabadiliko kiuchumi Tanzania
ReplyDeleteMdau wa USA
jamani watanzania kaani macho huyu mtu alietuma hii ishu ni tapeli wa kimataifa ameona akitumia njia ya kusema kuna kazi ugaibuni atawapata wengi kwani wtz wengi wanatamani kwenda nje ya nchi wakifiki maisha yao itabadilika lakini mimi ninavyoona huyu alie tuma huu ujumbe ni mtapeli kwelikweli amefikiria njia ya kuwapata wajinga akaona aseme ulaya kuna kazi hiyo ni ziro hakuna kitu utapeli mtupu asitupotezee muda hapa hatuna nafasi hiyo ya kujadili utapeli wa kijinga namna hiyo tumekushtukia mjomba
ReplyDeleteTafauti ya Ughaibuni na nchi za dunia ya tatu ni kuwa Ughaibuni kila siku wanaenda mbele kimaendeleo. Kuna watanzania sasa wanabiashara zao hapa na kazi nzuri tu kutegemea kipaji cha mtu. Kuna madaktari, mawakala wa mizigo (serengeti na wenziwe), kuna graphic designers (urban pulse na wenziwe) na kuna wapiga box. Mpiga box hana karatasi au elimu. Angalia sheria za viza za kila nchi. USA, UK, Canada na Australia bado wanataka wahamiaji. Nenda google angalia masharti yao kama unasifa wanazozitaka nenda ubalozini ukaombe viza. Hawa jamaa wakishaweka sheria basi wanazifuata. Usihonge mtu kwa viza. Kama sifa zote huna basi kilichobaki tena wewe mwenyewe unajua.
ReplyDeleteKUPIGA BOX....SIKIENI TU!
ReplyDeleteKazi kweli kweli......wengine tunafikiria kurudi nyumbani wengine ndio wanawaita wenzao waje huku, naungana na wadau waliotangulia kusema kuwa ULAYA SASA MAMBO YAMEKUWA MAGUMU, na wewe unayesema vijana wa Tanzania wamechoka zaidi naona una-generalize mno, mimi nimekwenda nyumbani Tz hivi karibuni, nimekuta rafiki zangu wengi tu wanafanya mambo makubwa hata baadhi yetu hapa ughaibuni hatuwafikii......kweli kama hapa ughaibuni una credentials za kutosha, utafurahia maisha lakini kama ndio mwenzangu na mie....mmmh! bora ubaki nyumbani! HALI HUKU NGUMU!
ReplyDeleteNdugu zangu watanzania ni wagumu kuelewa sana,aisee nimesoma comments zote nacheka sana jinsi uelewa wetu ulivyo chini,Huyu jamaa yeye anataka kuwasaidia watanzania wenzake,sasa mnaposema hana ndugu wala marafiki mna maana gani?kwani nyie sio ndugu zake?ndio maaana unakuta kwenye kazi anaajiliwa aliyeshikwa mkono na ndugu yake na haya yametokea sana hapa kwetu,sasa kaeleza vizuri kuwa mtu atakayemusaidia anaweza kumsaidia yeye pia kwa njia moja ama nyingine,na hii nilivyomsoma ina maanisha hata usipomsaidia yeye ina maana unaweza kuja saidia hata watoto wake,yaani kichwani kwetu kumejaa ufisadi tu,sasa nyie mnajuaje kama atakuwa tayari ameshawasaidia marafiki zake sasa anaamua kusaidia na wengine..,nchi zingine kama Kenya,Uganda,Ghana,Botswana na zingine huwa wanasaidiana pasipo hata kujuana na nimeyaona haya mara kwa mara,sasa mtanzania mwenzetu anataka kuwasaidia wengine watu mnaanza kuongea ongea tu kama wendawazimu.,na ndio maana hakuamua kuweka wazi nchi aliyopo mana kweli watanzania tumelogwa.
ReplyDeleteKumbe watanzania ni wabaya ivi, alafu eti watanzania tunapendana 'UNAFIKI TU' wengine mnasema ulaya kazi hakuna na data zenu za kinafiki kukatisha tu wenzenu tamaa mbona mmeg'ang'ania huko huko. Tunapendana kupeana bia tu na sahani za wali, watu wanataka maendeleo. Mwenzenu anataka kusaidia nyie midomo domo tu. Nyie mnaona ulaya dili kumbe wenzenu wanapachezea tu. Mwenzenu akienda roho zinawauma kwani hivyo viwanda mmejenga nyie? PENDANENI KIKWELI HACHA IZO
ReplyDeleteHiyo ni PHISHING!!
ReplyDeleteJamani mlioko ughaibuni huyu jamaa ni wa ukweli au kanyaboya mana kaficha nchi aliko, nimeshtuka kidogo mana wengi ni matapeli anatumia kigezo cha kusaidia ili apate anachotaka. Nahofia wengine yasije yakawakuta kama yalivyonikuta.
ReplyDelete