WANACHAMA wapya wa CCM wakiapa baada ya kukabidhiwa kadi za Chama, katika mkutano wa kutambulisha sekretarieti mpya ya CCM Taifa, uliofanyika Itigi mkoani Singida. . Jumla ya wanachama 70 walijiunga na 20 kukabidhiwa kadi kwa niaba ya wengine.
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) CCM, Nape Nnauye akicharaza gita la bezi huku Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mh. Martha Mlata akiimba, kwenye onesho la bendi ya Paradise Singers ya mjini Itigi katika mkutano wa kutambulisha sekretarieti mpya ya CCM Taifa, uliofanyika Itigi mkoani Singida. Kushoto ni mwanamuziki wa bendi hiyo Daniel Mtwane.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Chiligati akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CCM tawi la wanafunzi wa Chuo cha Biashara Singida, Hassan Msakamali, wakati Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM taifa, walipozungumza na wanachama wa tawi hilo, kwenye ukumbi wa FDC mjini Singida juzi. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
WAJUMBE wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) CCM, kutoka kulia, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) John Chiligati, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Katibu wa NEC, Oganaizesheni Asha Juma Abdallah na Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba, wakisalimia wananchi baada ya kuwasili kwenye mkutano wa kutambulisha Sekretarieti hiyo, uliofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya CCM wilaya ya Manyoni mkoani Singida.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM (Bara) John Chiligati, akizungumza na wanachama wa CCM tawi la wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Singida, katika ukumbi wa FDC mjini Singida

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...