Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhan Khijjah (kushoto) afafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi za kusaini hati ya msaada wa shilingi bilioni 1.2 ( sawa na Euro 500,000) kutoka kwa Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mheshimiwa Jacques Champagne de Labriolle(kulia) leo jijini Dar es salaam . Msaada huo umetolewa na Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika la Maendeleo la Ufaransa(AFD) kwa ajili ya kuendeleza sekta ya maji nchini.Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhan Khijjah (kushoto) akibadilishana hati ya msaada wa shilingi bilioni 1.2 ( sawa na Euro 500,000) na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mheshimiwa Jacques Champagne de Labriolle(kulia) leo jijini Dar es salaam . Msaada huo umetolewa na Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika la Maendeleo la Ufaransa(AFD) kwa ajili ya kusaidia kuendeleza sekta ya maji nchini.

Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam

Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika lake la Maendeleo la Ufaransa (AFD) imetoa msaada wa msaada wa shilingi bilioni 1.2 ( sawa na Euro 500,000) kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya maji hapa nchini Tanzania.

Msaada huo ulitolewa jana jijini Dar es salaam na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mheshimiwa Jacques Champagne de Labriolle wakati wa sherehe fupi za kusaini msaada huo zilizofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Uchumi.

Balozi huyo alisema kuwa msaada huo unahusu kusaidia maswala ya kiufundi katika kuendeleza mpango wa maendeleo ya sekta ya maji katika miradi inayofadhiliwa na wahisani mbalimbali likiwemo Shirika la Maendeleo la Ufaransa(AFD).

Alisema kuwa madhumuni ya mpango wa kuendeleza sekta ya maji (WSDP) ni kupunguza kiwango cha umaskini kwa kuwawezesha wananchi wengi kupata maji safi na salama yanayozingatia viwango vya ubora wa afya na mazingira.

Balozi huyo aliongeza kuwa kupitia Mkakati wa Kukuza uchumi na kupunguza umaskini wa Tanzania (MKUKUTA) unaweka mkazo juu ya huduma ya maji na udhibiti wa sekta hiyo katika kufikia malengo ya milenia ambayo ni kupunguza idadi ya watu wasio na maji safi kwa kiwango cha nusu ifikapo mwaka 2011.

Alisema kuwa AFD inampango pia wa kusaidia miradi ya maji katika miji ya Bukoba na Musoma ambayo inatarajia kuanza mwanzoni mwa mwaka ujao na kuongeza kuwa mchango wa AFD kwenye kapu la sekta ya maji hivi sasa ni Euro milioni 30 sawa na shilingi bilioni 52.5.

Mheshimiwa Jacques Champagne de Labriolle aliongeza AFD imejipanga kusaidia utunzaji wa mazingiara ya Ziwa Victoria ambalo linakabiliwa na madhara yanayotokana na ongezeko la idadi ya watu katika maeneo ya Mwanza, Kisumu na Jinja.

Alisema kuwa misaada ya ufaransa katika sekta ya maji safi na taka na usafi wa mazingira ni sehemu ya mpango mzima wa kuendeleza miundo mbinu ya kiuchumi na kijamii nchini Tanzania na nyingine za Afrika Mashiriki.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhan Khijjah alisema kuwa bado wananchi wote hawajapata maji safi na salama , hivyo msaada huo utasaidia kuendeleza kasi ya Serikali ya Tanzania kuhakikisha wananchi wengi wanapata maji safi na salama ifikapo 2025.

Alisema kuwa bila maji safi na salama maendeleo yanataendelea polepole na hivyo kusababisha uwepo wa matatizo mbalimbali ambayo yatasababishwa na mlipuko wa magonjwa mbalimbali yanayotokana na ukosefu wa maji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2011

    Muwe mnaweka wazi kama ni msaada au ni mkopo. Manake hivi karibuni kuna picha mlituwekea kichwa cha habari kinaona yesha tumepata msaada lakini ndani inaonekana ni deni. Haya madeni tutayalipa ni vizuri yakawekwa wazi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...