Benki ya Rasilimali ya Tanzania,yani TIB,katika kipindi cha mwaka 2010 ilipata faida kabla ya kodi ya shilingi bilioni 3.6 ikilinganisah na faida ya shilingi bilioni 2.9 iliyopatikana mwaka 2009.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Isidore Shirima
baada ya kufungua ofisi za benki ya TIB mkoani
humo kwa niaba ya Waziri wa Fedha
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo,Bw. Peter Noni  alisema ijuma kwamba kiwango hiki cha faida ni ongezekobla shilingi million 700 au asilimia 24 ikilinganishwa na kiwango cha kilichofikiwa mwaka 2009. Waraka mizania wa benk ulendelea kukua kutoka shs bilioni 167 mwaka 2009 hadi shs bilioni 244 mwaka jana.
Bw. Noni alisema katika sherehe za uzinduzi wa makao makuu ya kanda ya kasikazini ya Arusha na tawi la TIB Arusha  kwamba  kukua kwa  waraka mizania kulitokana na ongezeko la mtaji wa shilingi bilioni 50 na ukuaji wa mikopo ambayo ilifikiwa kiwango cha shilingi billion 106 (bada ya kutoa tengo la mikopo sugu) kutoka shilinhi bilioni 82 mwaka 2009(sawa na ukuaji wa asilimia 29).
Alisema kuwa kuna mpango mkakati unaolenga kutoa mikopo kufikia shilingi billion 1,099 ifikapo mwaka 2015. “Mpango mikakati wetu unalenga kutoa mikopo kufika bilioni 1,099 ifikapo mwaka 2015.tunatarajia ongeseko kubwa mikopo ys viwanda,kutokana na nia yetu ya kuwekeza zaidi kwenye viwanda vya usindikaji ili kukuza soko la bidha za wakulima,wafugaji,na wavuvi ambalo pia litawahakikisha bei nzuri na ongezeko la kipato”,alisema Bw. Noni.
TIB,pia inalenga utali,ujenzi,madini,miundombinu na maeneo ya viwanda na masoko.Kata hivyo mafanikio ya uwekezaji katika viwanda utategemea sana uwekezaji wa serikali katika  sekta ya umeme na usafirishaji.
Wageni waalikwa na maofisa wa TIB kwenye shere hizo
TIB kanda ya kasikazini  na tawi la benki Arusha vitatoa huduma mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro,  na Singida.Aidha,inje ya Dar Es salam, benki imeanza kutao huduma katika kikoa ya Mwanza,kagera,Shinyanga,Tabora na Mara kupitia office za kanda na tawi la Mwanza ambao inatarajiwa kufunguliwa siku chache zijazo.mkakati wa benki ni kufungua office ya kanda  na tawi Mbeya ifikapo mwisho wa mwaka hu, kanda zingine mbili ifikapo mwaka 2015.

Mwaka jana TIB ilitoa mikopo ya asilimia 30  katika sekta ya kilimo na usindikizaji kulinganisha na asilimia 25 ya mwaka 2009. “Sekta nyingine zilizokopeshwa ni pamoja na Mawasiliano na Uchukuzi,asilimia 12,Nishati ASILIMIA 8,Utali na Mahotel i asilimia 18,Viwanda asilimia 5 na sekta nyinginezo asilimia 26.Bw.Noni alisema kwamba mikopo hi ilitolewa kwa vikundi mbalimbali ambapo ofisi ya kanda   ya kazikazini  ina jumula ya asilimia 21,wakati kanda ya ziwa ina aslimia 17 na zinazobaki zimetolewa na Makao makuu kwenye waraka mizania,mikopo yenye jumla ya shilingi bilioni 88,(83%), ni ya muda wa kati na mfupi.

TIB benki pia itatoa huduma zote za kibenki kama zile zitolewazo na benki za biashara kupita kampuni yake tanzu TIB corporate bank ili kufikisha huduma kwa watu wote.
Katika drisha ya kilimo iliyoanzishwa Mei 2010 baada ya beki kupewa  bilioni 22,kutoka serikalini.hadi  kufika April 2011,maombi ya mikopo yalitimia 166 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 107. Miradi 49 ndiyo iliyoidhinishwa kati yake 15 ni ya makampuni,28 ya SCCOS na 6 asasi ndogo za fedha. Jumula ya mikopo mingine ya shilingi bilioni 12.6 iko mbioni kuidhiniswa.kutokana na idadi ya waombaji,Dirisha la kilimo la shilingi bioni 20 zimeongezwa na serikali.
Maofisa wa TIB wakitoa maelekezo kwa wageni
Kuanzia mwaka 2010 TIB imeanzisha huduma ya karadha ya fedha ambapo benki inakopesha mkulima binafsi kwa kumnunulia kifaa malumu ambacho atalipia kidogo kidogo kutokana na makubaliano.Mteja anatalajiwa kuwa mwaminifu kwa kutimiza wajibu wake.TIB ina mtaji wa shilingi  bilioni 92.14 kwa sasa ambazo hazitoshi mahitaji ya raia wanaomba mikopo.

Yeye waziri wa fedha , Mh. Mstafa Mkulo alisema serilkari iko mbioni kuhakikisha kwamba benki hii ina timiza mipango mikakati yake kwa ufanisi. Mkulo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hiyo alisema wako tayari kuiwezesha TIB ili eweze kufungua benki ya maendeleo ya kilimpo,ambapo wakulima wengi nchini watafaidika.

Akisoma hotuba ya waziri Mkulo  bada ya kufungua tawi na office ya kanda rasmi kataika viwanja vya Mount Meru Hotel, mkuu wa mkoa wa Arusha,Mh Izidoro Shirima  alisema kuwa President Jakaya Kikwete akizindua benki hii mwaka jana aliahidi bilioni 400 ambazo zitaiwezesha TIB kukubariana na mahitaji mbalimbali ya wananchi .

Kwa niaba ya bodi ya benki, Professor Emmanuel Lyakurwa, aliomba wananchi wote kutumia fursa hii wakabuni miradi ya kilimo ili wasaaidiwe kuondokana na umasikini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...