Ndugu Watanzania,
Kwa niaba ya Uongozi wa Watanzania wa Washington State, tunapenda kutoa
shukurani zetu za dhati kwa mahudhurio yenu katika sherehe za Muungano
zilizofanyika Jumamosi iliyopita pale Eritrean Hall. Shughuli ilifana sana.
Taarifa ya Mapato: Mlangoni tulikusanya $1025, mnada wa mavazi yaliyotolewa na
dada Asia $100. Hivyo mapato yetu yalikuwa $1125.
Matumizi: Tulilipa ukumbi $700, usafi wa ukumbi $100, muziki $300. Jumla ya
matumizi ni $1100.
Angalizo: 1) Vinywaji vilinunuliwa vya $ 400 na mauzo yalikuwa $410. Vinywaji
vingi vilibaki. 2) Tulitumia $ 466 kutoka mfuko wa TanzaSeattle kulipia
chakula.Kwa ujumla hatukutengeneza faida.
Tunawashukuru kwa upendo na umoja mliouonyesha, kwani bila kujitolea kwenu
tusingelifanikiwa kulipa madeni na kuburudika.Tunawaomba muendelee na moyo huo
wa upendo, hasa katika shughuli zetu zote zinazokuja.
Changamoto tuliyonayo mbele ya safari: Kwa nini tuendelee kulipia ukumbi kwa
wenzetu? Je jumuiya haiwezi kufikia kuwa na ukumbi na sisi tukakodisha? Majibu
ya maswaki haya yanakuita wewe Mtanzania uje kwenye jumuiya tusaidiane.
Ni watakie heri ya kazi,
Kedmon Mapana
Katibu


Hongera kamati/Uongozi kwa kutoa taarifa muhimu na kuja na wazo la kuboresha shughuli za umoja wenu na pengine kuongeza kipato cha jumuia.
ReplyDeleteMambo ya fedha huwa mara nyingi sana yanaleta migogoro, mara nyingine isiyokuwa ya msingi. Taasisi nyingine, na hata huko nyumbani wajifunze kutoka kwenu na kutoa taarifa kama hizi mapema.
Mdau, Norway
WATANZANIA UMOJA WETU NI MGUMU KUWEPO KWA SABABU NYINGI SANA.
ReplyDelete1-HATUNA UTAMADUNI WA UMOJA ANGALIA WAHINDI MAJEMATINI.
Kwa hiyo mimi nategemea wabongo waanze kujadiliana kwa kujichunguza nini ni tatizo nilipata kuona balozi wa tanzania uk sasa yuko marekani kwenye YOU TUBE AKISEMA wawe na ukumbi kama wa wahindi yaani WABONGO waanzekufikilia kuwa na ukumbi hilo aliwezekani kwa sababu wewe tangia unasoma shule uliisha changia hata watoto yatima au uliisha watembelea wazee na kuwasaidia hakuna BASI HATUWEZI KUFANYA UMOJA ILA UMOJA WETU NI KUANGALIA FULANI ALIKUJA NA BMW X5 NA ALIVAA VIZURI FULANI AMEKONDA MNAPOTEZA MUDA KITU KIZURI NI KUPIGANA KILA MTU AWE NA UWEZO BINASFI SIO UJAMAA ILA NI UBEPALI
Haina maana kutoa taarifa ni ufisadi haukufanyika. Inawezekana sana mahesabu yamechakachuliwa!!!
ReplyDeleteMimi naunga sana kutoa taarifa, transparency siku zote ni muhimu. Ila wazo ni kwamba hao watu waliokuja kwenye mkutano bwana Mapana I'm sure wana email address, kwahiyo ungewatumia taarifa kwenye email zao badala ya kutoa taarifa dunia nzima.
ReplyDeleteSidhani kama mtu aliyeko S Africa au Korea anataka kujua jana Washington walikuwa na mkutano watu watatu na walikunywa chai ya rangi na chapati na gharama yake ilikuwa dola tatu..
I could be wrong, I guess brother Michuzi considers everything
alo weee dogo mashauzi mithupu. nakumaindi ww mbona umebania meseji yangu vipi? afu punguza bange aloo jua kali sasa. meseji sent
ReplyDeleteacha acha ubisho dogo