Ndugu Watanzania,

Kwa niaba ya Uongozi wa Watanzania wa Washington State, tunapenda kutoa
shukurani zetu za dhati kwa mahudhurio yenu katika sherehe za Muungano
zilizofanyika Jumamosi iliyopita pale Eritrean Hall. Shughuli ilifana sana.
Taarifa ya Mapato: Mlangoni tulikusanya $1025, mnada wa mavazi yaliyotolewa na
dada Asia $100. Hivyo mapato yetu yalikuwa $1125.

Matumizi: Tulilipa ukumbi $700, usafi wa ukumbi $100, muziki $300. Jumla ya
matumizi ni $1100.
Angalizo: 1) Vinywaji vilinunuliwa vya $ 400 na mauzo yalikuwa $410. Vinywaji
vingi vilibaki. 2) Tulitumia $ 466 kutoka mfuko wa TanzaSeattle kulipia
chakula.Kwa ujumla hatukutengeneza faida.
Tunawashukuru kwa upendo na umoja mliouonyesha, kwani bila kujitolea kwenu
tusingelifanikiwa kulipa madeni na kuburudika.Tunawaomba muendelee na moyo huo
wa upendo, hasa katika shughuli zetu zote zinazokuja.
Changamoto tuliyonayo mbele ya safari: Kwa nini tuendelee kulipia ukumbi kwa
wenzetu? Je jumuiya haiwezi kufikia kuwa na ukumbi na sisi tukakodisha? Majibu
ya maswaki haya yanakuita wewe Mtanzania uje kwenye jumuiya tusaidiane.
Ni watakie heri ya kazi,
Kedmon Mapana
Katibu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2011

    Hongera kamati/Uongozi kwa kutoa taarifa muhimu na kuja na wazo la kuboresha shughuli za umoja wenu na pengine kuongeza kipato cha jumuia.

    Mambo ya fedha huwa mara nyingi sana yanaleta migogoro, mara nyingine isiyokuwa ya msingi. Taasisi nyingine, na hata huko nyumbani wajifunze kutoka kwenu na kutoa taarifa kama hizi mapema.

    Mdau, Norway

    ReplyDelete
  2. WATANZANIA UMOJA WETU NI MGUMU KUWEPO KWA SABABU NYINGI SANA.
    1-HATUNA UTAMADUNI WA UMOJA ANGALIA WAHINDI MAJEMATINI.
    Kwa hiyo mimi nategemea wabongo waanze kujadiliana kwa kujichunguza nini ni tatizo nilipata kuona balozi wa tanzania uk sasa yuko marekani kwenye YOU TUBE AKISEMA wawe na ukumbi kama wa wahindi yaani WABONGO waanzekufikilia kuwa na ukumbi hilo aliwezekani kwa sababu wewe tangia unasoma shule uliisha changia hata watoto yatima au uliisha watembelea wazee na kuwasaidia hakuna BASI HATUWEZI KUFANYA UMOJA ILA UMOJA WETU NI KUANGALIA FULANI ALIKUJA NA BMW X5 NA ALIVAA VIZURI FULANI AMEKONDA MNAPOTEZA MUDA KITU KIZURI NI KUPIGANA KILA MTU AWE NA UWEZO BINASFI SIO UJAMAA ILA NI UBEPALI

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 04, 2011

    Haina maana kutoa taarifa ni ufisadi haukufanyika. Inawezekana sana mahesabu yamechakachuliwa!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 04, 2011

    Mimi naunga sana kutoa taarifa, transparency siku zote ni muhimu. Ila wazo ni kwamba hao watu waliokuja kwenye mkutano bwana Mapana I'm sure wana email address, kwahiyo ungewatumia taarifa kwenye email zao badala ya kutoa taarifa dunia nzima.

    Sidhani kama mtu aliyeko S Africa au Korea anataka kujua jana Washington walikuwa na mkutano watu watatu na walikunywa chai ya rangi na chapati na gharama yake ilikuwa dola tatu..

    I could be wrong, I guess brother Michuzi considers everything

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 04, 2011

    alo weee dogo mashauzi mithupu. nakumaindi ww mbona umebania meseji yangu vipi? afu punguza bange aloo jua kali sasa. meseji sent

    acha acha ubisho dogo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...