Habari Ankal Michu,
Naomba uniwekee hii story hapo kwenye Globu ya Jamii kuhusiana na yaliyonipata na naomba wadau wanisaidie mawazo faster.
Niliagiza gari aina ya Suzuki escudo toka japan na kuipitishia bandari ya mombasa kwa sababu ambazo zinajulikana,nikimaanisha kukwepa usumbufu kwenye hii hapa ya Dar es salaam,sasa kila kitu kikaenda faster hapo Mombasa gari ikawa cleared.
Kufika boarder ndo mambo yakaanza kuwa magumu,gari ilikuwa na all original documents na invoice yake ikionyesha kwamba gharama za manunuzi na kusafirisha ni $ 4,500 kwa escudo ya 2002,jamaa hawa wa TRA pale boarder ya tanga wakasema hiyo bei ni ndogo hivyo ikawa uplifted to a higher price na kuchajiwa ushuru wa 6.4 M,ikawa hamna jinsi tukalipa huo ushuru.
sasa kwenda kutoa gari baada ya kuilipia jamaa wakazui wakidai kuwa mkanda wa hii gari una lebel inayoonyesha kuwa gari hii ni ya mwaka 2001 hivyo inatakiwa kulipiwa uchakavu,same time wao ndo waliokagua documents na kijiridhisha kwamba gari hilo ni la mwaka 2002 na kubambika ushuru wa 6.4m lakini sasa wanasema ni ya 2001 na wanadai ili wai-release gari tutoe rushwa ya laki Saba,documents zote zipo na zinaonyesha gari ni ya 2002,jamaa wameng'ang'ania gari na Mimi inanibidi nisafiri weekend hii tayari ninayo return ticket ready kwani nilikuwa tu hapa kwa likizo na hivyo sina muda wa kufight for my rights.
what should I do here?
Mdau wa Ughaibuni.
Naomba uniwekee hii story hapo kwenye Globu ya Jamii kuhusiana na yaliyonipata na naomba wadau wanisaidie mawazo faster.
Niliagiza gari aina ya Suzuki escudo toka japan na kuipitishia bandari ya mombasa kwa sababu ambazo zinajulikana,nikimaanisha kukwepa usumbufu kwenye hii hapa ya Dar es salaam,sasa kila kitu kikaenda faster hapo Mombasa gari ikawa cleared.
Kufika boarder ndo mambo yakaanza kuwa magumu,gari ilikuwa na all original documents na invoice yake ikionyesha kwamba gharama za manunuzi na kusafirisha ni $ 4,500 kwa escudo ya 2002,jamaa hawa wa TRA pale boarder ya tanga wakasema hiyo bei ni ndogo hivyo ikawa uplifted to a higher price na kuchajiwa ushuru wa 6.4 M,ikawa hamna jinsi tukalipa huo ushuru.
sasa kwenda kutoa gari baada ya kuilipia jamaa wakazui wakidai kuwa mkanda wa hii gari una lebel inayoonyesha kuwa gari hii ni ya mwaka 2001 hivyo inatakiwa kulipiwa uchakavu,same time wao ndo waliokagua documents na kijiridhisha kwamba gari hilo ni la mwaka 2002 na kubambika ushuru wa 6.4m lakini sasa wanasema ni ya 2001 na wanadai ili wai-release gari tutoe rushwa ya laki Saba,documents zote zipo na zinaonyesha gari ni ya 2002,jamaa wameng'ang'ania gari na Mimi inanibidi nisafiri weekend hii tayari ninayo return ticket ready kwani nilikuwa tu hapa kwa likizo na hivyo sina muda wa kufight for my rights.
what should I do here?
Mdau wa Ughaibuni.
uncle wabongo nao ni chakachua sana ndio maana hata watendaji wetu huwa hawatuamini kwa uongo misiwalaumu hao ni sisi wenyewe tunajiharibia sabaabu ya kufoji mambo pole sana
ReplyDeleteKama unahisi upo sahihi ripoti kwa wakubwa
ReplyDeletekawape pesa za moto tu kukomesha hali hiyo. ndo mana uchumi haukui kwa sababu ya watu wachache kama hao hawaourudisha nyuma. pole kaka
ReplyDeletePole sana Mdau
ReplyDeleteTafadhali naomba uwasiliane na Meneja wa Mkoa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa namba 027 2647786 ambaye atakutatulia tatizo lako mara moja na kukupa maelezo ya hakika
Duh mie nashangaa huo ushuru tu 6.4m duh hatari ila yote tisa ninachotaka kuonyesha 10 kuwa hii nchi yetu tunayoita Tanzanzia tusahau kuendelea kwasababu kama munasema CCM ndio hawawezi kazi hata chama chengine kiingie kazi ipo kubwa sana kuweka mambo sawa kama tunavyofikiria na hapa ndipo watakapofeli manaake Tanzania kila sehemu kuna ufisadi kuanzia kwenye kucha mpaka kwenye nywele hatari sana hii
ReplyDeletebandugu kwa kuokoa muda tu, wape tu hiyo ela uchukue gari yako uende, lakini nenda mwenyewe kapatane nao usimtumie agent, maagent wengi wanatengeneza mazingira, tatizo la bongo unaweza ukataka kwenda juu na huyo wa juu kumfikia mpaka kwa ela, so ni yale yale. system nzima imeoza
ReplyDeletesasa kama unasema u don't have time to fight for your rights it means u are waiving ur rights..na kama ndio hivyo,soln ni kutoa hiyo laki saba,si hautaki ur rights!!!t seems u dont have time,u actually dont give a shit...this is sooo disappointing
ReplyDeleteKama kwenye mkanda wa agari imeandikwa 2001 na wewe una documents zinaonyesha Gari ni ya mwaka 2002 ...hi ni kama hadithi ya kuuza cheni ya gold fake na kulipwa hela bandia.
ReplyDeleteat some point i dont see the logic ya watu kutolea gari Mombasa eti wanakwepa usumbufu Bandari ya Dar wakati mwisho wa siku usumbufu zaidi uko mipakani maana huko ndio watu wanapisha magendo kila siku
Dude lipa hela uondoke zako kubali tu u are screwd/screw urself
Next time pitishia gari Dar achana na kupeleka gari mombasa
Kaka pole sana na mimi yamenikuta hivyohivyo katika bandari ya zanzibar inaonyesha huo ndio mchezo waliugunduwa TRA sasa hivi wanaangalia kwenye mkanda lakini kila nikipima naona sio sawa sbb ile lebo yakwenye mkanda niyamanufacture na pengine huomkanda ulitengenezwa 201 sasa mimi pia gari ninayotumia hapa kwenye mkanda imeandikwa 201 lakini serikali ya hapa imeandika ni gari 202!kwakweli TRA tanzania inawarudisha nyuma watanzania wenzake na huu mchezo wakwenye mkanda naona sasa hivi ndio wameutengeneza lakini wadau tunajihangaisha kuandika hapa sbb tunachoandika hakijadiliwi na viongozi wa serikali!lakini wanaturudisha nyuma sana na ndio maana wawekezaji wa nje wanapata kuendelea kirahisi sbb sisi tunabanwa!mimi hii ni gari ya nne sasa likitoka hili linakuja lingine!mtu mmoja tu anakupangia anavyotaka yeye!
ReplyDeletepole sana mkuu. hata mimi yalinikuta hayo hapa TRA Dar wakati wa kutoa bandarini. Niliongezewa kodi ya uchakavu na VAT. Nilijaribu ku appeal bila mafanikio. Ushauri toa hio laki 7 uachane nao ni rahisi kuliko kulipishwa tena. Mimi sikupewa nafasi hio. Hii ni kawaida atu wanakata mikanda.
ReplyDeleteukitaka halali bongo itakula kwako, we wakatie hela yao mambo yaende faster. sisi mbona tumeshazoea ndo bongo yetu kaka. hospitalini, vyuoni, polisi n.k bile kukata kitu kidogo utakoma.
ReplyDeletewe wakatie tu hata mungu atakusamehe kwa kuwa unawahi maswala yako bana!
Bora ungetoa hiyo laki saba mambo yakaisha la sivyo utajuta kwa nini umepeleka gari..mie yalinikuta hayo japo Gari langu halikuwa na umri zaidi ya miaka 10, lakini jamaa wa getini pale bandaaring wakadai eti nimelipa ushuru mdogo wakati nimelipa hukohuko TRA..Jamaa nuksi wao wanaendesha Ma Prado wewe ukiingiza ki-Rav 4 wanatoa macho wakutoze rushwa..na rushwa haitaisha bongo mpaka usumbufu uangamizwe.
ReplyDeletePole swahiba ila unaweza kwenda ofisi za TRA Tanga au hapa makao makuu na ukawaeleza mkasa wako wakakusaidia kama unayosema ni kweli. na kama wamekuomba laki saba, basi fika upanga tu pale PCCB wao wataziandika namba na mtaongozana kwenda kuwapa moto. hakika kama wameomba rushwa hiyo ni wanaharamu ila kama nawe unatudanganya basi wewe ni mwendawazimu
ReplyDeleteMichuzi hebu i-forward hii kwa JK.
ReplyDeleteKwa ufupi hii nchi imeoza na watu pia wameoza. Miaka mingi iliyopita nilikuja kutembea Tanzania kutoka masomoni. Sasa wakati ule kulikuwa na sheria mgeni alipa airport charge kwa dola na mtanzania anaishi ughaibuni naye alipe dola. Sasa wakaniuliza kama nilikuja kutembea nilipojibu ndio tu wakanigeuzia kibao wanataka dola 25 kama hivi. Sasa mimi ni mwanafunzi tu na nchi ninayosoma ni masikini haina hata kazi wala dola sasa mimi dola nitazipata wapi. Wakaniekea bati hapa husafiri mpaka utupe dola. Ilibidi nifichue dola nilizokuwa nazo ili nisafiri kurudi masomoni. Sasa sijui ile pesa iliingia serikalini au alikula mtu. Tatizo la magari ni kuwa ughaibuni kuna aina mbili za data za magari, kuna mwaka wa kutengezwa gari na mwaka wa "registration". Sasa mkanda kwa magari ya Japan utakuwa ni mwaka wa kutengenezwa. Baadhi ya wakati hii miaka inatafautiana. Kwenye documents huwa wanaandika registration number. Kuhusu bei za TRA walizotathimini magari haziendi na nchi husika. Sijui wanatumia kigezo gani katika kupanga bei. Ughaibuni bei za magari zinategemea na model, mileage, ajali na mtengezaji. Sasa TRA wao wanatumia kigezo gani?
ReplyDeletePOLE KAKA......INABIDI JAMAA WAENDE SHULE KIGODO..KWA KAWAIDA, GARI LIKITENGENEZWA BAADA YA MWEZI WA JUNE, HUWA LINAANDIKWA KUWA NI LA MWAKA UNAOFUATIA. KWA MFANO LEXUS ILIYOTENGENEZWA JUNE 2001, ITAANDIKWA KUWA NI YA MWAKA 2002....VERY SIMPLE. INAWEZEKANA HAWA JAMAA WANAJUA ILA TU WANATAKA KUWAIBIA. WABONGO BWANA, KWA NINI MSITUMIE INTERNET KWA VITU KAMA HIVI, NA BADALA YAKE MNATUMIA KWA VITU VISIVYO NA MAANA KAMA FACEBOOK????...SHAME
ReplyDeletehei mkuu pole sana nimepata issue kama ya kwako mwezi march ilikua ni RAV4 Toka uk all docs & logbook stated that the car was registered in 2002,remember all the logbooks in the UK have the date which the cars were first registered not MANUFACTURED, so you have to pay bro caus TRA Wanabase kwa year of manufacture, ila pamoja na hilo nimeappeal kwa GENERAL COMMISSINER sababa waliuplift sana nategemea majibu kesho nitaku update ili ufate mkondo huo ila kalipe achana na hao wanataka rushwa wakupe qure ukalipie
ReplyDeleteNimesoma comments zote na sioni kama hii rushwa itakomeshwa Tanzania shida ni sisi waTanzania nafikiri tunakubaliana na hao wapokea rushwa if something is wrong is wrong even if you try to make it right 100 times it will still be wrong stop encouraging them. Mimi nakubaliana na anonymous aliyesema mpigie Mkuu wa TRA akipata malalamiko mengi eventually atafanya kitu lakini mambo ya kuwa tunalipa pesa kuharikisha vitu sio haki hata wewe unayetoa rushwa ni mkosaji kama aliyedai.
ReplyDeleteje tutafika na hii nchi yetu kwa jinsi wanaovyoiangamiza hawa wakuda?
ReplyDeleteMaofisa wa TRA wamekosa common sense, utu na hawana ubinadamu,ni watoto wa wakubwa,hakuna wa kuwaambia chochote, si mkuu wa nchi wala wadanganyika,wao ndio wanaamua wanavyotaka hakuna sheria wala mjadala unapofika ofisini kwao,maamuzi ya mwisho wanayo wao, period.Ukitaka kuwajua rudi bongo baada ya kuwa ughaibuni kwa mwaka mmoja(masomoni ,nk) na uombe msamaha wa kodi wa kontena lako,utajuta maana utalipa zaidi ya hata ungelipa ushuru-kukomoana tu.
ReplyDeleteLakini mwisho wao utafika.
ila kwanini utoe rushwa unajua huu ni upumbavu...watanzania ni wapumbavu sana na mtu mnamshauri atoe rushwa badala ya kumwambia nani akamuone apewe haki yake....huu ni upuuzi laki saba..daaa hakuna haki kabisa.
ReplyDeletehawa wapumbavu wa TRA horohoro wamezoea, hawajui kama mikanda ni accessories mtu anaweza kubadili fashion au ikawa ni tarehe iliyotengenezewa mkanda, nani kawaambia model ya gari inaangalia kwenye mkanda? je gari ilifika haina mikanda? kila gari ina manufacturer plate kwann wasiangalie humo au na documents si wanazo wanadhani japan watadanganya? kuna mpumbavu 1 (Rama)yupo kitengo cha TBS hapo horohoro yan yeye amefanya TBS ni mradi wa tumbo lake. sasa tunawaandalia pesa za myoto
ReplyDeleteMnashangaa nini na ndio hao wana majumba kama ikulu. Ndio maana Mkapa aliamua kufuta kazi wote those days walikuwa wanhitwa income tax. Ni wezi wakubwa. Nusu ta kodi wanaweka mfukoni. Mimi ilishanikuta nikawakomesha nikawambia andika bill nikalipa sikuwahonga ata senti tano wezi wakubwa. Kuwakomoa wewe lipa ili mkose wote. Alafu mimi serikali inanishangaza. Mtu mshahara wake 1.5 ana mali kibao. Ukiuliza unaambiwa TRA huyo yaani jamii imehalalisha hawa jamaa watie mfukoni ela zetu za kodi!
ReplyDeletepole sana sheri zakodi zikowazi tatizo sio TRA ni company uliotumia kuclear hilo gari wanajua sheri za uingizaji wa magari naikitoke utata wao wanajua nin chakufanya sio kumuacha nteja alipe hela nyingi bila sababu na kuacha mzigo wake au gari lake bila sababu........sikunyingine au kama kuna mtu yeyote mwenye tatizo kama hilo nitumie email nitamsaidi stephencesma@ymail.com
ReplyDelete