Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO, limetangaza upungufu mkubwa wa umeme katika Gridi ya Taifa kuanzia Mei 19 hadi 26 ili kutoa nafasi ya matengenezo makubwa katika visima vya gesi ya Songo Songo.

Mgao huo mkubwa utainyima nchi umeme kwa saa 16 katika kipindi cha saa 24 kila siku.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi William Mhando alisema mgao unatokana na kusimamishwa kwa uzalishaji wa gesi asili iliyopo katika Kisiwa cha Songo Songo mkoani Lindi na wamiliki wa visima hivyo Pan African Energy Tanzania Limited, wakiwa na lengo la kuvifanyia ukaguzi na ukarabati ili kuboresha uzalishaji wa gesi kwa ajili ya kufulia umeme.

Tangu mwanzo wa mwaka jana gesi inayotolewa na kusafirishwa Dar es Salaam kwa matumizi ya umeme na viwanda imekuwa ikipungua kutokana na sababu za kiufundi.

Kutokana na kuzimwa kwa visima hivyo, vituo vya Songas, Ubungo Gas Plant na Tegeta Gas Plant vinavyotumia gesi asilia kufua umeme vitasitisha shughuli zake kwa siku hizo nne na hivyo kusababisha upungufu wa umeme katika Gridi ya Taifa kwa sababu umeme wa gesi huchangia karibu nusu ya umeme unaofuliwa katika vituo vyote nchini.

Mhando alisema kuanzia Mei 23 - 26 mchana, mgao wa umeme utakuwa megawati 300 kuanzia saa 2 asubuhi - saa 5 usiku na megawati 50 kuanzia saa 5 usiku - saa 2 asubuhi.

Kuhusu nishati ya maji, shirika hilo limesema hali ya umeme imekuwa nzuri siku za karibuni kutokana na mvua zilizonyesha na kuongeza maji kwenye vituo vya Kihansi, Kidatu na Pangani na kuwezesha uzalishaji umeme katika vituo hivyo na kupunguza makali ya mgao wa umeme kwa muda.

Hata hivyo, Mhando alisema kina cha maji katika Bwawa la Mtera bado kipo chini sana kwani hadi kufikia juzi kina cha maji katika bwawa hilo kilikuwa mita 691.18 usawa wa bahari wakati kina cha juu kwenye bwawa hilo ni mita 698.50 na kina cha chini ni mita 690.00 juu ya usawa wa bahari, hivyo tangu mvua zianze zimeongezeka sentimita 30 tu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 09, 2011

    kwa style umasikini hautaisha tanzania mpaka dunia itakapo kwisha,bora nchi iuzwe tu kila mtu apewe chake.huu ujinga huu????

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 09, 2011

    Usilaumu Tanesco, huo ndiyo mfano bora wa watanzania tunavyofanya kazi na tunavyoishi, hakuna tofauti ya Tanesco na maisha ya familia zetu katika majumba yetu. Maendeleo yanaanza nyumbani yanaingia offisini asubuhi. Sasa kama hujui familia yako ipo namna gani utajuwaje shirika linaongozwa namnagani?. Tumeshazoe mpaka nyumba idondoke ndiyo tunafanyia matengezezo, mpaka bomba lipasuke ndiyo linafanyiwa marekebisho, mapka mabasi yatuuwe ndiyo tamko linatoka. Huduma za Tanesco ni mfano mzuri wa maisha na jamii za watanzania zinvyoendeshwa. Kama hujali familia yako utajali watu ambao unawapa huduma? Tatizo ni sisi Watanzania na siyo Maji wala Gas.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...