Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (kulia) akibadlishana mawazo na Mwenyekiti wa Chama cha APPT Maendeleo,Peter Kuga Mziray (kushoto) wakati wa mapunziko ya kikao cha pili cha mkutano wa nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoendelea mjjini Dodoma.
Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais (mahusiano na uratibu),Stephen Wasira (kulia) akibadlishana mawazo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (utawala Bora), Mathias Chikawe(kushoto) na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima( wa pili kulia) na Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe(wa pili kushoto) wakati wa mapunziko ya kikao cha pili cha mkutano wa nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) akibadilishana mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd wakati wa kikao cha pili cha mkutano wa nne wa Bunge la Tanzania unaoendelea mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Aggrey Mwanri wakati wa kikao cha pili cha mkutano wa nne wa Bunge la Tanzania unaoendelea mjini Dodoma
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama(kushoto) wakati wa kikao cha pili cha mkutano wa nne wa Bunge la Tanzania unaoendelea mjini Dodoma
Naibu Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Aggrey Mwanri akijibu maswali mbalimbali ya wabunge jana Bungeni mjini Dodma wakati wa kikao cha pili cha mkutano wa nne wa Bunge la Tanzania unaoendelea mjini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria,Celina Kombani (kushoto) akibadlishana mawazo nje ya ukumbi wa bunge la Tanzania na Mbunge wa jimbo la Kigoma Kusini,David Kafulila (kulia) wakati wa mapumziko ya kikao cha pili cha mkutano wa nne wa Bunge la Tanzania unaoendelea mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha ,Gregory Teu (kulia) akibadlishana mawazo nje ya ukumbi wa bunge la Tanzania na Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za serikali za Mitaa, Augustino Mrema (katikati) na Mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini,Stephen Ngonyani (kushoto) wakati wa mapumziko ya kikao cha pili cha mkutano wa nne wa Bunge la Tanzania unaoendelea mjini Dodoma.Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kifimbo ChezaJune 08, 2011

    Kamanda! nahisi kichwa cha habari kimekosewa.... "BUNGUNI DODOMA LEO''' nahisi ulikuwa na maana .."""BUNGENI DODOMA LEO""" au?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2011

    Nchi za Kenya, Uganda na Rwanda Bajeti zao zinasikika moja kwa moja kwenye Mtandao. sisi Watanzania hatuna hata TV au Redio inayosikika "LIVE" kwenye mtadao AIBU sana hii.

    Magulu
    Germany

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2011

    MAgulu Aibu na wala sio ndogo tutabakia kuwa omba omba kama matonya

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2011

    Duh,Kumbe Mheshimiwa Mrema bado dawa ya Babu(Loliondo) haijamsaidia,maana naona bado ngozi haijakaa sawa.Tuzidi kuomba kwa Mungu amjalie Mh.Mrema apone.

    ReplyDelete
  5. As ante mdau nimerekebisha

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 09, 2011

    Kwani Mrema hayuko kwenye upinzani tena?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 09, 2011

    Anon Magulu usikonde google clouds fm mimi nimesikiliza bajeti yote. Na nipo Denmark pia wameshaanza live tv yao japo kwikwi kidogo lakini nawapa big5. Redio ni moja tu Tanzania CLOUDS FM. Unajua serikali imebanwa na haka kamuda subiri mpaka uchaguzi ujao upite ndio utapata National TV mtandaoni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...