MWANAMUZIKI NGULI WA AFRIKA KUSINI HUGH MASEKELA USIKU WA KUAMKIA LEO ALIGOMA KUPANDA JUKWAANI BAADA YA PROMOTA WAKE (JINA TUNAHIFADHI KWA SASA) KUSEMEKANA KUSHINDWA KUMLIPA KABLA YA ONESHO LILILOVUTIA MAMIA YA WAPENZI WA MUZIKI, HASA MAOFISA WA BALOZI MBALIMBALI PAMOJA NA WANANCHI KUTOKA KILA PEMBE YA JIJI KATIKA UKUMBI WA GOLDEN TULIP JIJINI DAR ES SALAAM.
MKURUGENZI WA MASOKO WA STANBIC BANK BW. SINGANO AMETHIBITISHA TUKIO HILO NA HIVI TUNAVYORUKA HEWANI WAKO PAMOJA NA HUGH MASEKELA HOTELI YA SOUTHERN SUN JIJINI DAR ES SALAAM TAYARI KUONGEA NA WANAHABARI KUELEZEA SAKATA HILO. JUHUDI ZA KUMPATA PROMOTA HUYO HAZIJAZAA MATUNDA HADI SASA...
Meneja wa Hugh Masekela akiwataka radhi wahudhuriaji kwamba Hugh Masekela hatotokea. Shoto ni promota Heri Bomani akiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa Stanbic Bank Abdallah Singano
Sauda Simba akipasha moto show hiyo.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Sauda Simba akipasha moto show hiyo.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA







Duh, hiyo kali wabongo nomaaaaaa!Ila jamaa naye yupo poa kawastukia kwa kutopanda jukwaani.
ReplyDeleteIla hii ni aibu kubwa sana na ni picha mbaya kwa Tanzania na watanzania kwa ujumla. Ukizingatia yale yalitokea kwenye BBA hivi juzi juzi na hilo nalo kwa mtu wa kutoka huko bondeni ni dhahiri kabisa itaonekana sisi watz ni watu wasio na maana.
Mdau.
Promoter alizania huyu kama wasanii wetu waliozoea kuwalalia?hawa wenzetu wanajitambua sana na hawataki mchezo hatakidogo kwa kitu kinachoitwa man made..
ReplyDeletekweli bongohambadiliki. Mnambebesha box Babu wa watu bila ya ujira?hivi mlidhani huyo ni Koffi Olomide ama soucus stars? big up hugh masekela watie adabu wadanganyika wenzangu
ReplyDeleteKweli Bongo tambararee..
ReplyDeleteHuyo Promoter huo Upuuzi wake angeufanya huku kwa Mabepari, mbona angefilisiwa mali zake zote kuwalipa fidia watazamaji waliopoteza muda na pesa zao..
Third world countries ni shida tupu katika nyanja zote!!
Imekuwaje tena huyu Sauda Simba, kagoma kutoa mapesa? Mwambieni TZ unafanyakazi kwanza baadae malipo. Halafu huu mtindo wa kununua tiketi mlangoni ndio matokeo yake hayo. Na hizi nyimbo zao za "I love you" tumeshazichoka, iteni vikundi vya kiTZ akuimbieni "Uswahilini kuna vituko". Ndio maana tunapata watu kama Bhoke kututia aibu kwa kuiga tamaduni sio zao.
ReplyDeleteWatanzania nasi tumezidi ubabaishaji,itakuwaje watu muandae tamasha na kufanya maandalizi kwa gharama pia watu kununua tickets,kikundi cha wanamuziki kusafiri hadi bongo na mwisho mshindwe kumlipa msanii ??hii ni aibu inayojirudia kuhusu Tanzania ikiunganishwa na aibu aliyotutia yule dada sura mbaya Bhoke kule sauz.Huyu Hughe Masekela siyo mwanamuziki cheap mnavyofikiria ni mtu profession na ana jina kubwa hata Marekani na Ulaya,Japan nk.na mtindo wa nchi za wenzetu mkikubaliana malipo kwanza ni hivyo na siyo ubabaishaji kama wa bongo,jamani bongo tutastaarabika lini ??kila jambo ni utapeli na ufisadi,kweli bongo tambarare.Aibu tupu !!!!
ReplyDeleteSauda alilipwa?
ReplyDelete