Vodacom Miss Kagera 2011 Janeth Abdul (kati)  akipozi baada ya kutwaa taji holi wikiendi hii katika klabu ya Linas mjini Bukoba . Shoto ni mshindi wa pili wa shindano la Miss Kagera 2011 Editha Sixmond na kulia ni mshindi wa tatu Sylivia Anatory, warembo hao wako katika picha ya pamoja na Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Afande Henry Salewi (aliyevaa suti nyeusi) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika shindano hilo.
warembo waliokishiriki kwenye shindano la miss Kagera 2011 wakishiriki kwenye chakula cha pamoja na wadau wengine baada ya shindano, chakula hicho kiliandaliwa na muandaaji wa onyesho la kumtafuta miss Kagera 2011 kampuni ya Angels Entertainment kwa kushirikiana na hoteli ya Smart iliyoko kattika manispaa ya Bukoba.
mmoja wa washiriki wa shindano la miss Kagera 2011 akipita mbele ya jukwaa akionyesha vazi la asili lililotengenezwa kwa majani ya migomba, shindano la miss Kagera lilifanyika katika ukumbi wa Klabu ya Lina's iliyoko katika manispaa ya Bukoba mwishoni mwa wiki.


washiriki wa shindano la miss Kagera wakionyesha umahili wao wa kusakata muziki, hizi zilikuwa ni hatua za aali za wao kujinadi kabla ya matokeo ya kumpata mrembo wa Kagera wa mwaka 2011 kutangazwa.

Mama Nice mmoja wa mdhamini wa shindano la kumtafuta miss Kagera na wawakilishi wengine watakaoshiriki kwenye shindano la Miss Lake zone, mdhamini huyo ndiye aliwapamba washiriki wa shindano hilo kupitia kampuni yake ya Nice Salon. Picha na Audax Mutiganzi wa Globu ya Jamii, Bukoba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...