Na Ripota wa Globu ya Jamii

BENKI ya Stanbinc inasikitika kufutwa kwa onyesho la mwanamuziki kutoka Afrika Kusini lililotegemewa kufanyika usiku wa jana Jumamosi kwenye hoteli ya Golden Tulip Dar es Salaam.

Onyesho hilo lilifutwa kufuatia mwandaaji ambaye ni Heri Bomani na Kamapuni yake ya Full Circle Africa Limited kushindwa kumlipa msanii kama walivyokuwa wamekubaliana awali.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika muda mfupi leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Abdallah Singano alisema “Tunasikitika sana kwa kufutwa onyesho hili ambalo tulikuwa tumedhamini tunategemea kuchukua hatua za kisheria kwa mwandaaji na Kampuni yake”.

Naye Mwanamuziki mwenye heshima kubwa ndani na nje ya Bara la Afrika Hugh Masekela alieleza kuwa amesikitishwa kutokana na mambo yalivyotokea.

“Tunasikitika sana kuja Dar es Salaam na kushindwa kufanya onyesho kama tulivyokuwa tumepanga kutokana na mwandaaji kushindwa kutimiza makubaliano yetu,

Tunaomba radhi kwa mashabiki wetu ambao walikuwa wamejitayarisha kuja kwenye onyesho hilo lakini napenda kuwaambia kuwa tutarudi tena Tanzania kufanya onyesho hapo baadaye” alisema Masekela.

Naye Singano aliendelea kwa kusema kwamba “Tunaomba radhi kwa mashabiki wote wa Hugh Masekela walionunua tiketi kuona onyesho hilo na hatimaye kufutwa”.

Singano anamalizia kwa kusema kuwa kwa wale wote walionunua tiketi za onyesho hilo wamtafute mwandaaji ili aweze kuwarudishia fedha zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 12, 2011

    "WHAT A PITY..!"

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 12, 2011

    Its is very embarrassing bwana Heri Bomani,kufanya ulichofanya kwa mwanamuziki anaeheshimika kama Hugh Masekela na wapenzi wake ni kujishushia hadhi wewe na kampuni yako kwa ujumla. Promoters wa kibongo acheni utapeli wa kishenzi, wenzetu wana- principals kwenye kazi zao, terms lazima zifuatwe, sio kuleta wizi wenu wakibongo, shwain we!

    ReplyDelete
  3. Ifike wakati wa kufanya kazi kwa ufasaha na uelewe mkubwa kwamba UBABAISHAJI UISHE TANZANIA kuanzia siasa, uchumi na michezo,sijui watu wa UTAMADUNI wapo wapi sasa.
    Kazi ya sanaa sehemu zilizoendelea ni utajiri sio hapa dar mtu anaibiwa sehemu yake ya muziki anakaa kimya
    WENGINE WASANIIwanapewa pilau na kuunga kampeni za siasa wakati anatakiwa kulipwa pesa yeye anapewa ahadi hewa jamani MZINDUKE WANAMUZIKI

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 12, 2011

    Tanzania tambarare!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 12, 2011

    STANBIC MKOME kazi kuchukua hela kubwa za riba lakini kudhamini tamasha mnashindwa???? shame on you!!!!! angalieni mfano wa makampuni ya simu na vinywaji!!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 12, 2011

    Pole sana Dada yetu Sauda, getting caught in this mess! Huyo promoter akamatwe achukuliwe sheria kali, hivi mbona tunaanza kuwa kama wanaija? am so dissapointed huyo mzee ataenda sema nini kuhusu Tanzania?
    Shame shame shame!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 12, 2011

    Hata center walioniuzia ticket wanasema fedha imeshapelekwa kwa mwaandaaji wa tamasha hivyo hawawezi kunirudishia. Yaani mi sina makuu wanipe hata elfu 25 tu inatosha. Walioniuzia ticket pia hawakuwa helpful kabisa, wameniambia kwa kuwa minshaliwa sasa nsitake kuongeza idadi ya waliozulumiwa.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 13, 2011

    Huyu Heri Bomani ni CEO wa Bank kubwa hapo Bongo. Yaani sijui inakuwaje kuleta huu uandaaji hafifu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 13, 2011

    this is incidence ya tatu na huyu promoter, and tumtafute wapi mbona hakuna contact information zake? mie ni mmoja wa hao watu tuliokuwa na ticket.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 13, 2011

    I trust this was beyond Heri Bomani control...seriously, I do not want to believe "amechakachua" ticket and sponsorship money.

    I pray he sought this out as soon as possible, for sake of his reputation.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 13, 2011

    Heri Bomani sio CEO wa benki yeyote sasa hivi. Alishafukuzwa KCB. Kwa hiyo ni mjasiriamali tu kama sisi wengine. Mimi nawashangaa zaidi Stanbic Bank. inakuwaje wameshindwa kutatua hili tatizo mpaka kujiingiza kwenye aibu kama hii. Heading ya tickets inasema "Stanbic Bank presents..." Na sio Heri Bomani presents.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 13, 2011

    Ninavyoambiwa ni kwamba Stanbick walisha mlipa Heri ikiwa ni pamoja na fedha za viingilio. Kisha Heri kaingia mitini! Eti huu ndio uBongoman!(Uboman!)Hata hivyo Stanbic wamekosea. They should have cared more about their brand/name being tainted by Heri's misadvanture. Tactically they ought to have settled with Masekela and resorted to court with Heri. They have lost more than they gain from this sad episode. What a pity!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...