Picha mbalimbali za muono wa hekaheka za maandalizi ya Uchaguzi wa wagombea nafasi ya Urais na Makamu wake katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha ( I FM) jijini Dar es Salaam unaotarajiwa kufanyika Juni 16,2011., kama baadhi ya makundi ya wanachuo wanavyoomekana leo. 
Wanaonekana wakipitapita maeneo ya chuo huku wakionekana kujadili baadhi ya mambo yao kwa vyovyote vile itakuwa ni juu ya uchaguzi huo kama unavyoona mambango haya yaliyofungwa juu ya miti katika maeneo ya chuo hicho
Mengine yana ujumbe kama huu yaani Mabadiliko yako hapa maneno ambayo yanafanana na yale ambayo rais wa Marekani alitumia japokuwa yeye alikuwa akisema "Mabadiliko Yanakuja".
(Picha zote  na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 15, 2011

    Kasheshe. Yaani huyu yuko chuo kama IFM na anaandika hivyo kwenye bango. 'The Changes Is Here'. Shame! Our education system is in the doldrums.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 15, 2011

    Ni mimi sijui kiingereza au?
    Hilo bango la mwisho linasema THE CHANGES IS HERE?
    I suppose it's not correct as it was meant to say 'THE CHANGES ARE HERE' OR 'THE CHANGE IS HERE'.wadau nisaidieni..

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 15, 2011

    THE CHANGES IS HERE ......
    I HAVE CHANGES YOU WAITING FOR....

    Ingawa nilisoma shule za kata lakini nina wasiwasi na Grammar ya hilo Tangazo, It is Broken English!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 15, 2011

    Changes is here? NO! "Changes are here" or " Change is here"
    I have changes you waiting for? NO! " changes you were/are waiting for"
    Vission? NO "Vision"

    Hivi kwa nini tunatupa kiswahili kung'ang'ania lugha za watu? Hawa wasanii hamna kura! Bango kubwaaa ukubwa wa pua si wingi wa kamasi, kura wapate wenye mabango madogo hapo juu, "ati listi" wamejitahidi lugha za watu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 15, 2011

    Nyie kweli ni wasomi maana "The changes is here" inaonyesha jinsi gani mlivyokwenda shule.

    Bongo tambarare!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 15, 2011

    Dah! Yaani hawa ndiyo wako IFM, na wanasimama kuomba uongozi; mweeeeh!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 15, 2011

    Kama anony wa tano alivyosema: Munadharau chenu na kuthamini cha watu wengine. Zuzu alimtelekeza punda wake wa miaka mingi kwa sababu ya Pickup. Kama wote tunavyojuwa Punda anahitaji majani tu. Lakini Pickup inahitaji: utaalamu wa kuendesha (kibali), ni deadly machine, inahitaji vipuri, mafuta, Utaalamu wa kukarabati nk. Baada ya miezi kadhaa punda aliuguwa na akafariki kwa kukosa matunzo. Na baada ya miaka michache pickup pia ikawa kibanda cha kulala kuku!Mmh!mambo.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 15, 2011

    Tumkaribishe Waziri wa Elimu atueleze maana yake nini? Mtu kafika chuo na anaandika hivyo. Ana mpango gani wa kuboresha viwango? Unajua cha kwetu ni kizuri tena sana. Lakini hali halisi ni kwamba Kiingereza ndiyo lugha ambayo inatumika zaidi kielimu duniani kote kielimu na hata wasomi wanaoanadika kichina, kijapani, kijerumani wanapanua usomaji wa mabuku na mapaper yao kwa kutafsiri kwa Kiingereza. Kwa hiyo hazina kubwa zaidi ya elimu imetunzwa katika lugha ya Kiingereza. Tusipokielewa kiingereza ni kwamba tumeamua kutoelewa na kutoeleweka katika dunia ya kisomi.Waziri atueleze ana mpango gani? Tatizo hili ni la siku nyingi na linazidi kukua

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 15, 2011

    Makosa ya upatanisho wa kisarufi na tahajia yanaonesha wazi kwamba shule hapo haikukaa vizuri sana.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 15, 2011

    Halafu hawa ndio wanataka kuendesha nchi hii. Kiswahili chenyewe wanaandika Atunaye ndio hatunaye hiyo. Wao kusikiliza muziki wa kimarekani. Wenzenu hawajui english vile vile. Mmarekani akifika chuo kikuu lazima apasi level zote za english ndio asogee mbele. Pamoja na kua english sio lugha yake. Nyie hamjasoma essay zao. Akiwa mhasibu na Advance diploma report ya hesabu na maelezo yake inabidi uwe mkalimali wa lugha za mataifa yote ndio ifahamike. Kazi kweli kweli!!!!!! Ngoja wagome usikie matusi yao.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 15, 2011

    WHAT A LOOSER!!!!

    Kama amevurunda kwenye hilo tangazo, Je akipata uongozi itakuwaje?
    Na uongozi wa chuo unakubali tangazo kama hilo bila kulipitia, aibu gani wanaonyesha hapo? tena mbele ya lango la chuo, wapita njia wote wanasoma!!

    Tusubiri kama atapita, tutaelewa hicho ni chuo cha ma loooooooo(..ser)

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 15, 2011

    ifm nayo ni zoa zoa tu ili mradi kuongeza idadi ya watu waliokwenda shule.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 15, 2011

    Na wewe hapo juu sio "Looser" ni Loser

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 15, 2011

    Huyo wa mwisho ana makosa mengi sana ya grammar, hapo kwenye mission alitakiwa aandike ''TRANSPARENCY'' na sio TRANSPARENT kutokana mtiririko wa maneno yaliyo kwenye mission hiyo!

    Nchi yetu inaelekea kubaya zaidi kuliko kule tulikotoka!!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 15, 2011

    WHAT!HALAFU ETI NI WANAFUNZI WA CHUO KIKUU,MAAJABU

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 15, 2011

    Direct translation from Swahili to broken English.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 15, 2011

    BTW Have you guys read the whole stuff?, yaani hilo bango mmelisoma had chini?, huko ndiko kuna broken kingereza hadi basi....mfano; TRANSPARENT badala ya TRANSPARENCY...kazi ipo.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 15, 2011

    woe is the state of our education !!

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 15, 2011

    Na wewe Anonymous wa 09:36 AM unawakosoa watu wanaoandika kiswahili kwa makosa ATUNAYE badala ya HATUNAYE na wewe umeboronga kiswahili sio ¨pamoja na KUA English sio lugha yake¨ neno sahihi ni ¨ pamoja na English KUWA sio lugha yake¨

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 16, 2011

    Guys we need to pray for this country, maana viongozi have not got a clue about what to do. Hata wanaopiga kelele kutaka kuchukua madaraka as an alternative government sijui kama wanajua watafanya nini wakipata madaraka- maana nao eti kwenye chaguzi za vyama vyao kuna rushwa na ubaguzi. Hivi Michuzi kweli huwezi kupata comments za Waziri wa Elimu kuhusu hilo bango? Please try and get him to comment.It would be interesting to hear what he has to say about what it means about the state of education in this country. Ukweli wa mambo hata kama Kiingereza si chetu, inabidi tukielewe vizuri kwa maana tunajifungia mengi kielimu na kimaarifa kama hatuelewi hiyo lugha. Kibaya zaidi ni kwamba hata aliyeandika hajui kwamba hajui na kwa hiyo hana mpango wa kufanya bidii ajue. Karidhika na hicho ambacho anadhani anajua na kajiandikia bango na kuanika kutojua kwake.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 16, 2011

    sasa niye woote mnaowakosoa hao waloandika hilo bango , sasa naomba niwaulize ili uwe kiongozi mzuri ni lazima ujue english ? mbona wachina hawajui kizungu mpaka raisi wao ? na kwanza hicho ni chuo cha IFM cha fedha na sio CHUO CHA KIDHUNGU ... SAWA ? MPOOOOOO

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 17, 2011

    Siyo lazima ujue Kizungu ili uwe Kiongozi. Lakini huyu si anasoma jamani na anasoma Institute of Finance Management. Niambie kitabu kimoja at tertiary level cha Finance au Economics au Accounting kilichoandikwa kwa Kinyakyusa au Kibondei! au Kiswahili. Lugha ya usomi kwa ngazi hiyo, na hili linazidi kushika kasi duniani kote, lugha ni kiingereza. Hata kwa wasomi wazungu continental Europe uelewa wa Kiingereza ni kitu kinachozidi kuwa muhimu siku hadi siku. Rais wa Uchina hajui Kiingereza? Sijui. Mimi najua Chou Enlai (PM wa zamani wa Uchina)alikuwa anajua na anajaua Kifaransa fluent kabisa lakini alikuwa natumia cha kwao Mandarin hadharani.Mimi ningekuwa Rais wa Tanzania nisingedharau Kiingereza ni muhimu kukijua ili kuelewa mambo ya Dunia. Lakini hadharani hata ningekwenda Uingereza ningezungumza Kiswahili as matter of national pride. Tusidanganyike eti hawa jamaa kwa vile wanazungumza Kichina hata wakiwa nchi za watu hawaelewi Kiingereza. Besides China nchi kubwa na ina wasomi na knoledge base kubwa ilioandikwa na kuhifadhiwa kikwao katika kila fani na hata hivyo Kiongozi wa kule asipoelewa ana competent interpreters wa lugha nyingi tu za kimataifa (Kiingereza, Kisawahili, Kifaransa, Kijerumani etc). Wenzetu take language and studying/learning in general very seriously- nashangaa kuna ndugu zangu mko tayari kusema huyu jamaa kaboronga lakini it is okay, it does not matter. Why bother kama mnaridhika na kitu sub-standard? Tukubali tu huyu jamaa katutia aibu hajui na hajui kwamba hajui na ni aibu kuanika kutokujua kwako hivi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...