 |
Maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yameanza rasmi jijini Dar es Salaam leo huku baadhi ya mabanda yakiwa katika hatua za mwishomwisho za kupanga bidhaa zao. Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Ramadhan Khalfan amesema kuwa maonyesho ya mwaka huu yatakuwa katika ubora wa hali ya juu kutokana na maboresha waliyoyafanya. |
Bidhaa zikiletwa maoneshoni
Baadhi ya wafanyabiasha wakiingiza bidhaa zao katika viwanja vya Maonyesho vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakiwasili uwanja wa maonesho
Baadhi ya wafanyabiashara wakiendelea kupanga vizuri bidhaa zao
Maandalizi ya mwisho mwisho. Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii
asante sana michuzi kwa hizi picha. nashukuru kwa kutuonyesha some of the things being displayed at the show. hilo jiko hapo chini ni lizuri. naona watanzania hatuna haja ya kununua some of these things overseas. sikujua vitu kama hivi vinaweza kupatikana nyumbani. michuzi endelea kutuonyesha more products.
ReplyDeletekweli, vitu vipo nyumbani, pesa yako tu
ReplyDeleteMichuzi naomba utuwekee contacts za hawa jamaa wa majiko, ili tuweze kuwasiliana nao.
ReplyDeleteMdau Richie