Meneja Mauzo wa TBL,Fimbo Buttallah akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa kutangazwa kwa uzindizi wa mashindano ya ngoma za asili kwa mwaka 2011 yatakayofanyika katika mikoa mitano hapa nchini.kulia ni Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager,Edith Bebwa.
Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager,Edith Bebwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar leo alipokuwa akizungumzia uzinduzi rasmi wa mashindano ya ngoma za asili yatakayofanyika katika mikoa mitano hapa nchini.kushoto ni Meneja Mauzo wa TBL,Fimbo Buttallah.

Kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha BALIMI EXTRA LAGER inatangaza rasmi ufunguzi wa mashindano ya ngoma za asili kwa mwaka huu wa 2011.
Bia ya BALIMI EXTRA LAGER imekuwa mdhamini rasmi wa mashindano haya kwa zaidi ya miaka saba sasa. Lengo kuu la kudhamini mashindano haya ni kushirikiana na wakazi wa kanda ya ziwa katika kuenzi na kulinda tamaduni za kanda alisema meneja wa bia ya Balimi Extra Lager Bi Edith Bebwa.

Vile vile ni njia moja wapo kwa wakazi kujipatia kipato cha ziada kupitia zawadi zinazotolewa na bia ya Balimi Extra Lager.

Mashindano haya yatajumuisha mikoa mitano Mwanza, Shinyanga, Tabora, Mara, Kagera na fainali kurudi tena jijini Mwanza.
Maboresho makubwa yamefanyika katika mashindano haya ya mwaka 2011 ukilinganisha na yale ya mwaka jana. Zawadi zimeongezeka mara dufu. Hii ni kuwapa changamoto wakazi wa kanda ya ziwa kushiriki zaidi kwenye mashindano haya ya ngoma za asili za mwaka 2011.
Kwa niaba ya TBL kupitia kinywaji chake cha Balimi Extra Lager tunawakaribisha wote kushuhudia michuano hii na vilevile waburudike na Balimi Extra lager. Zaidi tunavitakia heri vikundi vyote vitakavyoingia kwenye mashindano haya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2011

    Kwa nini kila jambo la maendeleo yaani mpaka mambo ya ngoma za kitamaduni utakuta mikoa ya Lindi na Mtwara haipo kabisa ??Yaani mikoa hii imesahaulika kwa kila kitu utadhani ipo katika nchi nyingine na siyo Tazania.Kila kukicha si magazeti si mitandao, kuona habari za mikoa hii ni ndoto kabisa sijui ni kwa nini???labda wadau mna mawazo ya kuchangia hapa.Ikibidi labda Msumbiji au Malawi zipewe mikoa hii ndipo itatambulika maana Tazania inonekana kuwa haijihusishi kabisa na mikoa hii karibu kwa kila jambo.Miaka ya nyuma ilikuwa mtu akipewa transfer kwenda mikoa hii kikazi anaamua kuacha kabisa na kazi yenyewe,naona watu hawa walikuwa na sababu tosha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...