Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwaonyesha waheshimiwa wabunge Kombe ambalo Ofisi ya Bunge imeshinda katika Maonyesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa kushirikisha taasisi mbalimbali za Umma kutoka barani Africa na kufikia kilele wiki iliyopita tarehe 23 Juni, 2011. katika Maonyesho hayo Ofisi ya Bunge imekuwa mshindi wa Pili katika nafasi ya banda bora kwa utoaji bora wa huduma hususani katika kuelezea Kazi za Bunge, Muundo wake, Mamlaka ya Bunge nk. Shoto ni Kaimu Katibu wa Bunge Bw. John Joel.
Picha na mdau Owen Mwandumbya wa Bunge
Picha na mdau Owen Mwandumbya wa Bunge
Jamani sasa tuleteeni picha za taasisi ambayo ilikosa kikombe.
ReplyDelete