Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Charles Singili (kulia) akibadilishana mawazo na mmoja wa wateja wa benki hiyo Charles Mamuya (kushoto) wakati wa program maalumu ya ‘Wiki ya Wateja’ inayoendeshwa na benki hiyo katika matawi yake kote nchini kwa wiki nzima kuanzia Jumatatu ya wiki hii kwa lengo la upata maoni juu ya utendaji wa benki hiyo.Katikati ni Meneja wa tawi la Masdo yalipo makao makuu ya benki hiyo Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Charles Singili (kushoto) akiwa katika dawati la Huduma kwa Wateja katika tawi la Masdol Dares Salaam jana akishiriki kutoa huduma na kupokea maoni juu ya utendaji wa benki hiyo kutoka kwa wateja katika programu maalumu ya benki hiyo ya Wiki ya Wateja anayoiendesha kwa wiki nzima kuanzia Jumatatu ya wiki hii katika matawi yao kote nchini.Wengine ni Hassani Magongo na Joyce Chabakanga (kushoto).
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Charles Singili (kushoto) akiwa katika dawati laHuduma kwa wateja katika tawi la Masdol Dares Salaam jana akishiriki kutoa huduma na kupokea maoni juu ya utendaji wa benki hiyo kutoka kwa wateja katika programu maalumu ya benki hiyo ya Wiki ya Wateja anayoiendesha kwa wiki nzima kuanzia Jumatatu ya wiki hii katika matawi yao kote nchini.Kulia ni mfanyakzi wa benki hiyo Joyce Chabakanga.

Na Mwandishi Wetu

BENKI ya Azania imedhamiria kuboresha utendaji wa huduma kwa wateja wake ambapo kwa wiki nzima kuanzia mwanzoni mwa wiki hii inaendesha program maalumu ya ‘Wiki ya Wateja’ kupokea maoni kuhusu huduma zao.

Menejimenti nzima ya Benki hiyo akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wao, Charles Singili imekuwa ikishiriki moja kwa moja katika mazungumzo ya ana kwa ana na wateja ikiwa ni pamoja na kugawa kipeperushi maalumu cha kujaza maoni kwa wateja husika.

Akizungumza kuhusu program hiyo, Singili alisema ni sehemu ya kuwashirikisha wateja wao na watanzania kwa ujumla katika kufanya tathimini ya pamoja ya utendaji wao.

Alisema ingawa wenyewe wamekuwa na tathimini yao ya ndani lakini waliona ni bora kushirikisha wateja na kupata maoni ya upande huo wa pili kwani wakati fulani unaweza kuona unakwenda sawa kumbe unapotea.

“Ni program tunayoifanya kwa mara ya kwanza na tumeona ni muhimu kwetu kupata tathimini ya nje hususani kutoka kwa wateja wetu na lengo kubwa ni kuangalia jinsi ya kujiimarisha kiutendaji”, alisema Singili.

Alisema mpango huo maalumu kwa wiki yote unaendeshwa katika matawi yote ya benki hiyo na kwamba sasa utakuwa utaratibu wa kawaida kwao.

Kwa upande wake John Maigu mkazi wa Dar es Salaam ambaye ni mteja wa miaka mingi wa benki hiyo alisema ni mkakati mzuri kwa benki hiyo na anaamini watapata mengi yatakayowasaidia kuinuka zaidi.

Alisema amekuwa mteja wa benki hiyo tangu ilipokuwa ikiitwa 1st Adili na kwamba ameendelea kushawishika kubaki na benki hiyo kutokana na huduma zao na uwezeshaji unaolenga kuinua watu wenye vipato vya chini.

“Ni benki inayoonekana kweli imedhamiria kufanya biashara ya kibenki kwani wamekuwa wakiimarika kila siku lakini kizuri zaidi ni ushawishi wao katika huduma na hiyo ndiyo inayonifanya niendelee kuwa mteja wao kwa miaka na miaka sasa”, alisema Maigu.

Wamiliki Wazalendo wa Benki ya Azania wanayoisimamia kwa miaka kumi ya kujiendesha na kiasi cha hisa wanazomiliki ni NSSF 35%, PPF 30%, PSPF 12%,LAPF 14%, EADB 6% wakati wadau wengine wa kawaida wa kitanzania na wafanyakazi wa benki hiyo wanamiliki 3% ya hisa za jumla za benki hiyo.

Kwa sasa benki hiyo ina mtaji wa sh. bilioni 19/- na kwamba tayari imefungua matawi saba katika maeneo mbalimbali nchini katika miaka kumi ya kujiendesha tangu ilipoanzishwa rasmi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...