Naibu Spika Job Ndugai akiwaamuru wabunge wa CHADEMA Tundu Lissu, Mchungaji Peter Msigwa na Godbless Lema kutoka ndani ya Bunge leo mara baada ya wabunge hao kuvunja kanuni ya Bunge ya kuongea bila ruhusa ya Naibu Spika.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha akisoma bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo Bungeni mjini Dodoma leo kwa mwaka wa fedha 2011/2012.
Godbless Lema ambaye ni msemaji mkuu wa kambi ya upinzani kuhusu wizara ya mambo ya ndani ya Nchi akisoma makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2011/2012.
Askari Polisi wa Bunge wakiwasindikiza wabunge wa CHADEMA Tundu Lissu (kulia) Mchungaji Peter Msigwa (kushoto) na Godbless Lema (wa pili kushoto) ili waondoke nje ya viwanja vya Bunge mara baada ya Naibu Spika Job Ndugai (hayupo pichani) kuwaamuru watoke ndani ya Bunge leo baada ya wabunge hao kuvunja kanuni za Bunge za kuongea bila ruhusa ya Naibu Spika. Wa pili kulia ni Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akiwasindikiza wabunge wenzake.
Askari Polisi wa Bunge wakiwasindikiza wabunge wa CHADEMA Tundu Lissu (kulia) Mchungaji Peter Msigwa (kushoto) na Godbless Lema (katikati) ili waondoke nje ya viwanja vya Bunge mara baada ya Naibu Spika Job Ndugai (hayupo pichani) kuwaamuru watoke ndani ya Bunge leo baada ya wabunge hao kuvunja kanuni za Bunge za kuongea bila ruhusa ya Naibu Spika.
Mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA) Godbless Lema akiingia ndani ya gari huku Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) akisubiri kuingia mara baada ya Naibu Spika Job Ndugai kuwaamuru watoke ndani ya Bunge leo baada ya wabunge hao kuvunja kanuni ya Bunge ya kuongea bila ruhusa kupata ruhusa ya Naibu Spika.
Askari Polisi wa Bunge wakihakikisha kuwa gari lililowabeba wabunge wa CHADEMA Tundu Lissu, Mchungaji Peter Msigwa na Godbless Lema linaondoka nje ya viwanja vya Bunge mara baada ya Naibu Spika Job Ndugai kuwaamuru watoke ndani ya Bunge leo baada ya wabunge hao kuvunja kanuni za Bunge za kuongea bila ruhusa ya Naibu Spika.Picha na Anna Nkinda - Maelezo
Kila mtu huwa anawasikia CCM wakipiga kelele bila ruhusa hadi mama yao Anna Makinda akikaribia kulia, leo mmeamua. Itakula kwenu,,,,nyie jichimbieni shimo tu.
ReplyDeleteCHADEMA Kupiga makelele na kupinga tuuu kila kitu kurukia rukia hoja ili kuvuruga mjadala ili mtolewe bungeni na hatimae muandikwe na kutolewa kwenye magazeti kila siku kitu ambacho mtu yeyeto anaweza pia kufanya haimaanishi huko ndiko kuchapa kazi,picha tunayoipata sisi wananchi ni kwamba hamjui mnachokifanya na kama mnajua basi mnatupeleka ndiko siko maana hayo siyo matarajio yetu kwa miaka5 tuliowapa na hamfai kutuongoza.......
ReplyDeleteHonestly, Chadema mnaudhi sasa! Watu watawaheshimu kama mtaheshimu bunge. Utaratibu wa kuongea bungeni unajulikana, kwa nini msisubiri nafasi zenu ili muweze kutumuia demokrasi ya nchi yetu kusema yale yanayowasibu?? With this attitude nobody is going to believe you, hakuna nchi inayotaka kuongozwa na viongozi wanaopayuka bila staha, be civil and you will earn respect, fuateni utaratibu uliowekwa. KURA YANGU HAMUIPATI NG'OOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO! WHAT A MESS FROM MISUTO TO TALKING WITHOUT ORDERS LIKE BIRDS. Hata nyumbani tunawafundisha watoto wetu kunyoosha mikono darasani na kusubiri mwalimu akuite jina ndiyo unaongea. PRACTICE WHAT U PREACH.
ReplyDeleteHivi hawa wamefanya ndalilo hiyo tabia yao ya kutoka nje ya bunge ama kwa kuamua au kufukuzwa? Nafikiri hii ni triki wanatumia ili waende mnadani wakatanue nyama choma bia pamoja na vimada maana kukaa bungeni wanaona wanachelewa matanuzi au watasinzia sasa bora kila siku walianzishe ili wafukuzwe watoke nje? Hivi wao ni wa chekechea kila siku wafundishwe kanuni?
ReplyDeleteHuwa sipendi siasa ila hapa kuna tatizo...Bahadhi ya viongozi wa bunge/bahadhi ya wabunge kuna wale wanafanya shughuli za bunge lakini bado "LEARNING ON THE JOB".Ni mawazo yangu michuzi..Tuna matatizo mengi sisi huku uraiani..bunge linapoteza muda kwa mambo ambayo siyo ya msingi..Hadhi ya bunge inashuka jamani nyie waheshimiwa.
ReplyDeleteDavid V
Siasa ni kama mchezo wa mpira,ukiwa nje ya uwanja ni vigumu kuujua ugumu wa mchezo,ila kwa ushabiki ni wakati wa kulaumu.Hivyo si CHADEMA au Speaker yupo sahihi wote wanamapungufu yao.Speaker anaongopa kuruhusu chadema watohoe yale yanayowakera suluhisho ni kuwatoa nje,CHADEMA nao wanaona kama wanaonewa ndio maana wanajaribu kuongea kinyume na utaratibu waliojiwekea.Kwa mvutano huo sie huku basi tena.
ReplyDeleteHizo kanuni za CCM ndio zimetutia umaskini na kuendeleza ufisadi hadi leo. Sio kitu cha kushangaza hilo kutokea , watanzania acheni uoga nchi haitabadilika kwa lelemama..
ReplyDeleteWACHAPAKAZI TUNAWAJUA, NA WAZEMBE TUNAWAJUA! WABUNGE JIHESHIMUNI KM MNAVYOJIITA WENYEWE 'WAHESHIMIWA' sasa kufuata tu kanuni mnashindwa, je kufuata katiba mtaweza kweli? Speaker naye ni mtu mzima hawezi tu kukurupuka akamfukuza mtu, lazima hawa wanaojiita 'WAPINZANI' wana shida wanatafuta sifa kwa wananchi, kwa maana nyingine, sifa gani hata kanuni zinawashinda, je mkipewa nchi nzima mtaiweza kweli, au ndo mtakuwa mnaleta tu fujo kila mara?
ReplyDeleteTO BE A GOOD LEADER YOU HAVE TO BE A GOOD FOLLOWER,,,,,YOU CAN NOT GIVE COMMAND IF YOU CANNOT TAKE ORDERS!!
ReplyDeleteNyie mnaosema chadema wavurugaji hamna akili mtaishia katika umaskini tuu mnatetewa mnasema chadema hawana akili nyie zimeganda wakomeni chadema tunaipenda pondeni mtajijuuuuuuu CHADEMA OYEEEEEEEEE
ReplyDeleteNaungana na mdau hapo bila kuparangana mtabakia kwenye umaskini nyie wanyamaze alafu iweje ndio maana wengine umaskini umewajaaaaaaa alafu manasema chadema hawana akili nyie ndio akili zenu matope mtadhulumiwa kila siku mtakaa gizani mpaka mwisho wa dunia,watajilimbikizia mali kama kawa,maisha yatapanda kila siku mnatetewa manaleta midomo mirefu ,CHADEMA tutawapa kura 2015 kama kawa ,haya hiyo EPA,RICHMOND mbona imeishia hewani??????? Watanzania fungukeni macho hawa CCM bila kuwapeleka resi tutaambulia umaskini kila siku
ReplyDeleteNimefuatilia bunge la jana kwa ukaribu mkubwa. Jinsi alivyowashirisha hotuba ya kambi ya upinzani mh. Lema na jinsi alivyosimama Lukuvi kutoa hotuba kupinga hoja za upinzani (CHADEMA). Kwa kweli Bunge linaendeshwa kwa ushabiki sana na kwa upendeleo mkubwa kwa chama tawala (CCM) na uonevu mkubwa kwa chadema. Kweli jana huyo naibu spika ndugu ndugai aliniudhi sana na kama uchaguzi ungefanyika leo CCM wangesahau kabisa kupigiwa kura kutokana na watu wengi tunavyo-symphathize na wanavyotendewa CHADEMA. CCM ndio wamekuwa wakiongoza kuzomea bungeni na kuwasha ovyo vipaza sauti, iweje leo hukumu itolewe kwa Mh. Lema, Lissu na Mbunge wa Iringa Mjini pekee. Uonevu mkubwa. Huu ni ushenzi kabisa.
ReplyDeleteMakelele ya CHADEMA ni kama ya kilabuni maana hamna kusikilizana na huwezi kuambulia point yeyote ya kuondoa umaskini kama mnavyodhani-mwisho wa kelele za kilabuni ni kulewa na kugombana...kuibiana,kusutana......na machafu yote hufuata. Hakuna muda wa kufikiri matatizo ya wananchi,ni kuangalia tuu kasoro za wapinzani wao bila kutoa mchango wao mpaka muda unakwisha. KURA ZITAWAHUKUMU...tumeshawaona HATUWAPI KURA NG'OOOOOOOOOOO mmeshindwa kazi...
ReplyDeleteNadhani mnaomtetea speaker hamkufuatilia bunge hilo lilowatoa wabunge wa CHADEMA kweli ni uonevu mtupu.Mimi ni CCM lakini Chama changu sasa kimezidi uonevu.Wao siku zote ndio vinara wa kuzomea na kupiga meza kwa fojo kama wabunge wa upinzani wanapochangia hoja lakini hawachukuliwi hatua yoyote bali kanuni za bunge ziko kwa CHADEMA pekee.
ReplyDeleteKwa ushauri wangu ni bora bunge likawa na watu wachache wenye busara na hekima na wanaojua nini wanafanya kuwawakirisha wananchi sio kwa sasa ambalo bunge halieleweki na Speaker na naibu wake ndio kabisa matatizo mengine nafasi hii hawaiwezi wajitahidi kuangalia wenzao katika nchi nyingine wanafanyaje. mfano hapa UK sijaona ujinga kama unaofanyika huko kwetu.
Chadema hawana akili wala wasijidanganye kuwa hivyo ndo watajizolea umaarufu.Kamwe hawawezi kabidhiwa nchi hii kwa jinsi walivyo wapayukaji.
ReplyDeleteTUACHILIE MBALI KELELE ZA VYAMA TUONGELEE ISSUE YENYEWE. POLISI WAMEUWA WATANZANIA KWENYE MAANDAMANO YA AMANI NA HUKO KWENYE MACHIMBO NYAMONGO NA KWENGINEKO. HAKUNA ALIYEFIKISHWA MAHAKAMANI, ANASIMAMA MBUNGE NA WAZIRI LUKUVI WA CCM KUSEMA HAKUNA ISSUE HAPO HIYO NI SAWA?.
ReplyDeleteYAANI MAISHA YA MTANZANIA YAMEKUWA YA BEI RAHISI KIASI KWAMBA WATU WANAUWAWA, HAMNA KESI MAHAKAMANI, WABUNGE CCM WANAWASAFISHA POLISI BUNGENI, WAKILALAMIKA CHADEMA OOH WABAYA!!! AU CHADEMA INAWATETEA WATANZANIA AMBAO NI WAJINGA KIASI KWAMBA HATA HAKI ZAO HAWAZIJUI?
MPAKA WAANDAMANE KAMA MALAWI WAHISANI WATUNYIME MISAADA NDIO TUELEWE WANACHOSEMA CHADEMA KWAMBA HUWEZI KUUA BINADAMU KAMA NG'OMBE?
HEBU TUACHE TARATIBU NA KANUNI ZA BUNGE KWANZA AMBAZO NI MALUMBANO, TUJIULIZE, CHADEMA WANA POINT AU HAPANA?
Tuondoe ushabiki kwenye ishu serious...
ReplyDeleteLukuvi alimkatisha Lema kwa mamlaka gani?????? HILI NDIO SWALi LA MSINGI
Someni hotuba ya Lema ambayo Lukuvi aliingilia(filibuster).
Msiconclude tu kuwa CHADEMA ni wakorofi, ukorofi wao unaletwa kiziwi na kipofu CCM ambaye anafikiri mabavu ndio suluhu....
Wandugu things are changing and the world is moving if CCM cant change then it is going to die...
We have to objective na kuipeleka hii nchi mbele...
wakulaumiwa sio chadema ni serikali iliyopo nchi inateketea mnataka chadema wafanyaje nini? lazima wafanye kila linalowezekana ili kieleweke kitaeleweka tu piga uwa
ReplyDeleteHAO UNAWAONA WANAPIGA MAKELELE WANAUCHUNGU NA NCHI YAO TENA SANA KITAELEWEKA TU HATA KWA MAKONDE LAZIMA TUJUWE MWEISHO WAKE
ReplyDeletekwa kwili sisi watanzania ni wajinga kupita kiasi na ndio maana tunaishia kukaa na giza, shida ya maji na matatizo chungu nzima yanayotusonga.JAMANI WATANZANIA AMKENI FUNGUKENI AKILI MUWAZE APO MBELE CHADEMA WAPO SAWA KABISA NA WANACHOFANYA.CCM HAWATAKI CHADEMA WASEME KASORO ZAO JUENI PALE BUNGENI NDO PA KUTOLEA MATATIZO YETU SASA WAKASEME WAPI JAMANI TUTADIDIMIZWA MPAKA LINI NA CHAMA TAWALA CHADEMA WANAWAPA CHALLENGE HAWA MAFISADI WAKONGWE.EBU FIKIRI HAO MAFISADI WAMECHUKULIWA HATUA GANI LEO HII ETI MTU KUZIIWA KUONGEA BUNGENI ATOLEWE NJE HII KITU INAKERA WATANZANIA MBONA CCM WANASIMAMA WANAONGEA BILA KUKATISHWA AU KWASABABU NI WANAFIKI WANAUNGA HOJA WAKATI HAPOHAPO ANALALAMIKA NA KUTOA SHIDA YAKE.CCM ACHENI UONEVU MUNGU HAPENDI JAMANI WEWE MUNGU INGILIA BUNGE HILI UWATANDIKE WAONEVU WOTE NA WANAOENDESHA BUNGE KIMABAVU HII SI DEMOKRASIA YA KWELI HAKI ITENDEKE.RAIS KIKWETE WAONEENI HURUMA CHADEMA MSIWAONEE HIVYO TWAFAHAMU YINYI NI WABABE LKN INAWABIDI MKUBALI CHALLENGE WANAZOWAPA HIYO NDO DEMOCRASIA.
ReplyDeleteCCM WANAJIFANYA WANAJUA KILA KITU KWA WINGI WAO WALIOKUWAPO BUNGENI CHADEMA KOMAENI HIVYO HIVYO MSIOGOPE KITU
ReplyDeleteache ushabiki ninyi mnaoponda chadema hahisi ninyi ni watoto wa mafisadi au mafisadi kabisaa.na wala hamna matatizo yoyote ndo maana mnasema hayo.Nchi hii kwamwe haitaendelea kama hawatakuwepo watu kama chadema hawaungi hoja kinafki.wanataka mambo yawekwe sawa sasa hawataki chadema waongee matatizo ya wananchi wanafikiri wameenda kuuza sura kama wao?chadema big up tunawapenda wanainchi wote afu nyie cuf naona mnataka kufungishwa ndoa ya pili na ccm mume wenu i hate cuf tatizo mnauchu wa madaraka kwanini msikubali tu kuongozwa mbona ninyi mliongoza kipind kilichopita jamani kuweni wastaarabu.huyo mzee cjui kwanini alichaguliwa keshajichokea maisha bungeni anatafuta nn hana ata haya eti cc hawapo kweny upinzani sasa mpo wapi cuf au ndo mnabembeleza ndoa ovyoooooooooooooo.
ReplyDeletenimekuwa nikifuatia bunge kwa makini sana na ni kwa mda mrefu.honestly chadema wanaonewa hawatendewi haki.ili bunge mheshimiwa SITA peke ake ndo alikuwa analiweza hakuwa na upendeleo wa kijinga,Ana mama angu jiuzulu tu huliwezi na hao kina job ndo kabisaa sijui nani kawapa ujasiri au kawaagiza waendeshe bunge kibabe kama bunge ilo ni la ccm peke yao kwel hii c siasa starabukeni wapendwa mnakera watanzania kuona mnawanyanyasa wawakilishi wetu huwa natamani kulia napoona mnawakataza wasiseme matatizo yetu mnaishia kuwasimamisha hao kina Lisu sasa watatusememe kina nani mnatupeleka wapi jamani hasa sisi tusiokuwa na uhakika wa maisha.hapana msifanye ivyo ondoweni upendeleo.na huyo anayesema eti daktari atafutwe ili kupima waheshimiwa anatakiwa aanze yy hakika yule c mzima wa akili keshajijua ndo maana anataka daktari aje ili athibitishwe kwa umma kuwa yy ni mwendawazimu huwezi kukurupuka tu na kuomba daktari mtu mzima ovyoo et kisa mama wa chadema kaongea vile yule mama aliongea kwa uchungu sana wenye akil timamu walimuelewa vizuri ww tu na kutaka sifa ndo ukassema hayo pole aibu yako hiyo.sasa nini maana ya vyama vyingi si ndo challenge zenyewe mnapewa na chadema mmezoea tu kuunga mkono hoja wakati tunakufa masikini ninyi mnakumbatia tu mahela na mashangingi.chadema wapo kimaslahi ya wananchi ndo maana wapo tayari kumwaga unga wao au maisha pia kwani mmewauwa wangapi wa chadema ninyi ccm wapuuzi watupu.mmeoza et mwajivua gamba aibu ya chama.
ReplyDeleteMpaka hapo ilipofikia sikuona kosa la chadema. Endekezeni ushabiki tu lakini nchi haiongozwi kidemokrasia. Mtakapojua maendeleo ni nini ndio mtaanza kumtafuta mchawi na itakuwa too late. CCM inangamiza nchi.
ReplyDelete