Kuwashirikisha Watanzania wanaoishi Ughaibuni (Diaspora)

Mhe. Bernard Membe
Mheshimiwa Spika, Wizara yangu tayari imeunda Idara ya Diaspora na tumefanikiwa kuwafikia kwa wingi Watanzania walioko nje kupitia mikutano na majukwaa mbalimbali na kupata maoni yao. Kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Rais wa Zanzibar ameunda Kitengo cha Diaspora kinachoongozwa na Naibu Katibu Mkuu ambacho kipo chini ya ofisi yake na tunashirikiana nacho kwa karibu sana. Aidha, yapo maelewano na wadau mbalimbali ikiwemo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Benki Kuu, Kituo cha Uwekezaji, Mamlaka ya Mapato, Shirika la Nyumba la Taifa, Mfuko wa Uwekezaji (UTT), Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii na wadau nje ya Serikali kama Benki za CRDB, Benki ya Exim (Tanzania), Commercial Bank of Africa, na Mawakala Binafsi wa Ajira (Recruitment Agencies). Maelewano haya yanasaidia katika mkakati mzima wa kujenga mazingira ya kisheria na kisera ya kuwezesha Diaspora kushiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, hatua iliyo mbele yetu ni kwa Wizara yangu kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwanasheria Mkuu, kujenga mazingira mazuri kwa wanadiaspora na kuondoa kero ambazo zinaathiri jitihada zao za uchangiaji katika maendeleo ya nchi yetu.  Hivi sasa Wizara zetu zinajiandaa kuwasilisha Waraka kwenye Baraza la Mawaziri, ili ujadiliwe na kisha kwa wakati muafaka, Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi kutakiwa kuwasilisha rasmi mbele ya Bunge lako Tukufu Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Uraia kwa majadiliano. Kwa kuwa mchakato wa suala hili unagusa Katiba, ni azma yetu kuona kwamba suala hili linakwenda pamoja na mchakato wa Katiba mpya. Ni dhamira ya Wizara yangu kuona suala la Uraia wa nchi mbili linazinduliwa sanjari na Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2011

    Sikusudii kulaumu ila tu nataka kuweka point kuwa serikali naona inaposema watanzania wa diaspora huwa wanamaanisha watanzania waishio UK tu. Maana ndio huku tu ambako ni kama mara tatu sasa serikali wameweza kufanya mikutano na kuonana na watanzania. Kuna wengi tuko katika nchi mbali ya UK na serikali haijajaribu kutufikia kama inavyofanya UK, tuko wengi tu katika nchi ambazo haziko mbali na UK na tena tukowatanzania wengi tu katika nchi hizo lakini serikali wala balozi zetu hazijawahi kuja na idea ya mikutano kama hiyo inayofanywa UK.

    Kama nilivyosema sikusudiii lawama ni maoni yangu tu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2011

    Hao diaspora ni akina nani? Michango yao mbona haionekani kwenye bajeti? Mbona wanapotuma pesa zao hatuoni makato yaliyotokana na fedha hizo?. Tanzania mbona inazidiwa hata na Malawi kwa watu wanaotuma pesa makwao hii inatokana na taarifa za kimataifa zilizopo. Hatuna imani na kitengo hiki kama kweli kinawaunganisha watanzania waliooko huko. sisi wananchi watanzania tunaomba kitengo hiki kifutwe.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 23, 2011

    wewe anonymous wa sat.jul. 23,08.37.00 pm 2011 elimu yako finyu sana. wewe unataka serikali itoze kodi remittance za watu kwanini. infact wananchi wengi wanafaidika na hizo pesa. who are wananchi. wananchi ni watu wenye kuunda hiyo serikali kwahiyo wakifaidika serikali pia inafaidika. wewe ondoka kwenye hiyo cacoon yako ama sivyo dunia itakuacha nyuma. unajua unaweza kuwa na phds lakini fikira zako zikawa finyu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 24, 2011

    Dunia nzima inafahamu kuwa remittance ni mojawapo ya vyanzo vya mapato katika nchi zinazoendelea. Ndugu yangu unayepinga wazo hilo wewe sio diaspora, sisi tunawafuta diaspora. Sio watu wanaosubiri nchi ijengwe halafu wanakuja na maneno kuwa ni wawekezaji kutoka diaspora. Na kuleta maneno ya huko ulaya ambayo hayafanyi kazi katika mazingira ya Afrika. Elimu ni ngumu kumfanya mtu aelewe kama hakwenda shule. Tungekutana ungejua Elimu yangu ukapima na ya kwako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...