Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo Nyumbani kwa mpigania uhuru na kada wa CCM,marehemu David Zimbihile(80)  wakati wa mazishi yake yaliyofanyika Muleba jana  jioni.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu  mzee David Zimbihile wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika Muleba jana jioni.Mzee Zimbihile aliyewahi kuwa mbunge na kushika nyadhifa mbalimbali katika Chama Cha Mapinduzi alizikwa kwa heshima zote kijijini mwake Muleba, mkoani Kagera
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la kada wa CCM na mpigania uhuru, mzee David Zimbihile wakati wa mazishi ya kada huyo mkongwe(80) yaliyofanyika Muleba,Mkoani Kagera
Mwenyekiti wa CCM ,Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua katika kaburi la mpigania uhuru na kada mkongwe wa CCM  David Zimbihile wakati wa mazishi yake yaliyofanyika Muleba,mkoani Kagera jana jioni.Marehemu Zimbihile alianza harakati za ukombozi wa mwafrika nchini Kongo(DRC) ambapo alifanya kazi kwa karibu na Marehemu Patrice Lumumba na baadaye kupitia vyama vya wafanyakazi alikutana na Marehemu Kwame Nkurumah na hatimaye alirejea nchini Tanzania kuendelea na harakati hizo Picha na Freddy Maro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...