![]() |
Marehemu Timothy Eugen Haule |
Ulikuwa Nguzo na msaada wetu mkubwa kwetu sisi wanao na familia kwa ujumla tunakukumbuka kwa mengi mpendwa baba yetu kwani ucheshi, hekima na busara zako tutazienzi daima.Pengo ulilolicha kwetu ni kubwa mno ila kwa nguvu za kristo tumesimama imara.
Unakumbukwa sana na Mke wako Mpenzi Mrs. Josephine Haule, watoto wako Dorah,Sophia, Beatrice, Magreth, Oliver, Juliana, na Suzan. wakwe zako Gereson, Zawadi, Anikija, na Deo Pia unakumbukwa na wajukuu zako Elinory, Jenice, Victoria, Asharose na Abdieltimothy Kaka, Dada zako na ndugu jamaa na Marafiki, Majirani zako waOceanroad Flats.Tunajua kimwili hauko nasi ila kiroho tuko nawe daima baba mpenzi
Kutakuwa na misa ya shukrani nyumbani kwa Marehemu T. E. Haule
Ocean road Flats leo Jumatatu Tarehe 25 Julai, 2011 saa 11 jioni na nyote mnakaribishwa.
RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA MWANGA WA
MILELE UMWANGAZIE APUMZIKE KWA AMANI
AMEN
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...