Habari za leo Kaka Issa Michuzi na watendaji wote wa Glob ya jamii, kwanza kabla ya yote napenda kuchukua wakati huu ki pekee kabisa kuwapongeza sana kwa kufanya kazi nzuri sana ya kutupa habari popote Duniani pia imekua changamoto kwangu binafsi na kufikiri na kutafakari zaidi kuhusiana na maswala ya kublog..Pili napenda kuwapa pongezi sana kwa nyie kuchukua tuzo mbali mbali katika Tanzania Blogs Awards ambayo iliisha hivi karibuni. Baada ya salamu hizi basi naomba unipe nafasi nipate kujieleza mimi ni mwanalibeneke kama wanalibeneke wengine lakini hasa blog yangu imejikita katika kuhabarishana habari ambazo zinatokea kila kona ya Tanzania ndio maana nimeita jina la Latest news Tz. Nilikua naomba msaada wako wako wa kunitambulishia blog hii kwa watanzania wote Natanguliza shukurani zangu kwako na kwa Timu nzima ya Libeneke la Globu ya jamii.
Jina La Blog: Latest News Tz
Habari wadau wote popote Duniani, Tunapenda kuwakaribisha katika Libeneke la Latest News Tz.. Ambapo mtapata taarifa nyingi kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania Bara na visiwani.. kama unahabari usisite kututumia kupitia latestnewstz@yahoo.com.. Asanteni sana.
Latest News Tz tumekufikia. Link: http://www.latestnewstz.blogspot.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...