Jaji Mkuu Mh. Mohamed Chande Othmani(kulia) akipata maelezo  ya ukarabati na ujenzi unaoendelea wakati alipotembelea Mahakama ya Kisutu jijini Dar.
 
NA MAGRETH KINABO - MAELEZO
 SERIKALI imeamua kufanya ukarabati mkubwa katika Mahakama  ya Hakimu  Mkazi ya Kisutu jijini  Dar es Salaam,  ambapo itakuwepo mahabusu ya wanawake, ikiwemo ya watu maalumu wa jinsia hiyo (VIP) unaokadiriwa kugharimu  sh. milioni 750.
 
Hayo kasema  Msanifu Mwandamizi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania(TBA),Deogratias Chubwa, ambao ndio wasimamizi wa ukarabati huo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya kibiashara ya kimataifa kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere DaresSalaam.
   
  Hata hivyo ,Chubwa alisema gharama hizo zinaweza kuongezeka kutokana na  uamuzi uliofikiwa baada ya kikao cha TBA na Maofisa wa Magereza kufuatia mahakama hiyo kutokuwa na eneo la mahabusu wa jinsia hiyo ambao walikuwa wanawekwa maofisini baada ya kufikishwa mahakamani hapo, ikiwemo kuongeza eneo la kuegesha magari. mengi zaidi ya awali.
  
  "Tunasimamia ukarabati mkubwa unaohusisha vitu vingi katika mahakama ya Kisutu, ambapo tunafanya ukarabati ya mifumo ya maji taka ambayo ilikuwa haifanyi kazi,kujenga uzio, mgahawa mpya mfumo mzima wa umeme na kuweka Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEKNOHAMA), Hivyo jengo la Mahakama ya KISUTU litakuwa la kisasa," alisemwa Chibwa.
 
Aidha Chubwa aliongeza kuwa  ukarabati huo, unafanyika kufuatia jitihada za Rais Jakaya Kikwete za kuboresha hadhi za mahakama mbalimbali nchini.
 
  Alisema ukarabati huo ulianza mwaka jana na ulitarajia kukamilika Aprili mwaka huu,lakini umeshindikana kutoka ongezeko la eneo hilo la mahabusu na maegesho ya magari, hivyo unatarajia kukamilika Oktoba Mwaka huu.

  Chibwa aliongeza kuwa fedha za ukarabati huo zinatolewa Mahakama kupitia Serikaliuu.
  Alisema  awali walishasimamia ukarabati wa mahakama za mwanzo katika mkoa wa DaresSalaam, ambazo ni Kigamboni,Mbagala, Kinondoni,Magomeni,Mazense, Temeke na Ukonga, uliokuwa ukifanyika kuanzia mwaka 2006 hadi mwaka 2008.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2011

    Michuzi,mbona Mahakama ya kinondoni haionyeshi kama ilishawahi kufanyiwa/kurekebishwa hata siku moja,au watu waliweka fedha mifukoni??????????

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 09, 2011

    mahabusu ya VIP? Mtu ameshawekwa mahabusu kwa kuwa ana hatia bado anapewa u-VIP? ok! sisemi mengi nikapigwa mawe bure!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...