Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscer Shelukindo akizungumzaa na wachezaji wakati wa mashindano ya Kuunda timu ya Mkoa wa Ki nondoni yanayoendelea katika Klabu ya Mwanese Dar es Salaam.
Baba na Mtoto wakishindana wakati wa mashindano hayo,Kulia ni Baba, Mayaula Muhagama kutoka timu ya Jaba ya Mwananyamala na Mtoto Majaliwa Mayaula wa timu ya Shoko.
MASHINDANO ya Pool Safari Lager katika hatua za awali,timu za Shoko na Topland zaonyesha ubabe wa kuongoza mashindano hayo katika Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Timu ya Shoko yenye makazi yake Mbezi Beach inaongoza kundi A, mara baada ya kuzifunga timu zote za kundi hilo wakati wa mashindano hayo kwa kucheza michezo minne na kushinda yote ikifuatiwa na Meeda ambayo inamichezo 4,imeshinda 3 na kupoteza 1.
Timu zingine ni Mkwajuni inamichezo 3,imeshinda 1 na imepoteza 2,Ubungo inamichezo 3,imeshinda 1na kupoteza 2 na Jaba ina michezo 4 na imepoteza yote.
Wakati kundi B, Topland yenye makazi yake pale Mikumi jijini Dar es Salaam inaongoza kundi hilo ambapo inamichezo 4,imeshinda 3 na imepoteza 1,ikifuatiwa na 4Ways ambayo imeshinda michezo 2 na kupoteza miwili.
Timu zingine katika kundi hilo ni Bahama ambayo imeshinda michezo 3, imepoteza 2,Madrid inamichezo 3,imeshinda 1na imepoteza 2 na Mlalakuwa inamichezo 3,imeshinda 1na imepoteza 2.
Katika hatua za wawali timu mbili zinatakiwa kuondoka na timu 8 kuingia hatua ya robo fainali.
Mashindano hayo yanafanyika katika Klabu ya Mwanese Mabibo jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa TBL kupitia bia ya Safari Lager.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...