ankal akijumuika na wadau katika mpunga wa harusi msikiti wa Swahilina uliopo Kinondoni block 41 baada ya Swalat 'Jumaa
Katika kupiga mpunga kuna mikao aina kwa aina
Na waandaaji wanapochelewa hali huwa hivi....maana mikono ishaanza kukauka ati
Ewaaa... tonge nyama sasa. Biriani swaaaaafi kabisa hili..
bado ndizi tu na mfuko wa rambo. huto tukombe ni halua hiyo...ya dessert






Mh! Haka kasahani katawatosha kweli? Halafu huo mkao wako unaonekana hujala mpunga muda mrefu. Hizi fiesta noma.
ReplyDeleteAnko huyo mkao wako matata sana , naona unavinya mpunga uku kidole kimoja kinapiga hatua karibu karibu na minofu hilipo! ahhahah hapo anasubiriwa mmoja tu ajidusu kugusa nyama .ahhaa
ReplyDeletemdau paris
Karne hii bado kuna "zunguka mbuyu"? Michuzi umesahau ndizi na kifuko cha rambo.
ReplyDeleteHapo mjanja nani? Maana naona nyama ziko kati lakini mjanja kazisukumia kwake kiaina. Duuh Ankal mjanja wewe.
ReplyDeleteMikono wananawa au? Kwa sababu naona wengine wanashika pua na mokono hiyo hiyo itaenda kwenye sahani? Salaaale.
ReplyDeleteMmpunga huo unanikumbusha Maulidi ya nyumbani. Enjoy!
ReplyDeleteJamaa linakula peku peku huku limevaa saa? Ustaarabu gani huu?
ReplyDeleteulaji huu unatakiwa uzoefu hasa kwa wale tuliozoea vijiko ni kazi kwelikweli.
ReplyDeletepiga mpunga macho kwenye nyama hahaha ankali kumbe ushakula chumvi nyingi nakuona yasmini zimeanza kuchanua kichwani hahaha
ReplyDeletehivi ankali muda mwingi unakuwa kwenye minuso ya nje hivi shangazi yangu unamuacha apike alafu huonekani unakula kona
Baabuu naona umepiga koti iko ficha nini dani yake?
ReplyDeletepili pili che? ndiji che? yote dani ya koti. fuko nayo upoo?
Ankali Ndizi iko wapi??
ReplyDeleteMbona hukutuhabarisha vizuri, nani aliyeowa au kuolewa? Huyo mdau aliyevaa t-shirt anaonyesha msikiti anaujua siku za mpunga tu. Kumbe Ramadhani tayari, ndio maana harusi nyingi siku hiza!!
ReplyDeleteHuyo jamaa aliyevaa saa inaonekana ni moto wa kuotea mbali na aliwapeleka kisawasawa.
ReplyDeleteAnkal hivi kweli ni ustaarabu kulia ndani ya nyumba ya mungu? Mimi ni mkirsto,nauliza tu kwa sababu sikutegemea kitu kama hiki,watu mle humo humo then mnasalia humo humo,muogopeni mungu.
Inaelekea uliupania huo mpunga kuliko unavyopania kuangalia mechi za bwawa la ndubwi.......
ReplyDeletekwa kweli,twende mbele na turudi nyuma. Haina maana kwakua babu zetu walikaa chini wakila na sisi tufanye hivyo hivyo..huwezi kukanyaga hapo na viatu alafu ukaweka sahani hapo. Mikoni inapita sehemu nyingi kweli na hasa kwa joto tulilonalo na bakteria wengi, kwa nini vijiko havitumiki? kama ni watu wengi ni kweli tunahitaji kulia kwenye sinia lakini mikono mingi ni vizuri kutumia vijiko kupunguza kontakt na mikono ya wengine ambayo hujui kama imeoshwa vizuri.Mkao,inawezaje kula mbele ya wenzako na miguu iko juu? Ningependa tujiulize kidogo..chakula kinaitaji heshima and usafi..
ReplyDeleteAucle safi sana peleke ze ubwabwa!!huyu mshikaji anaeuliza kuuhusu kula msikitini mbona hata sie kanisanitwala sana tu?kwani hapo umeona kuna vileo?Mi ni mlutheri na makanisa yote tunaliamo labda hilo lako la kakobe ndo lina masharti kibao
ReplyDeleteMdau Manchester!
Mijitu mengine bwana Yesu kristo alikuwa anagawa mikate kwa vipande tugawane makanisani sasa leo unauliza kula kanisani? wewe vipi umesikia Chakula kwani kichafu?
ReplyDeleteKula msikitini kwani kuna ubaya gani jamani,kuna watu hawana makazi nchi za kiarabu kama wasafiri wanakaa msikitini kula chakula ni jambo la Kheri sana wala sio kilevi,na kanisani mbona watu huwa wanalishwa mkate,sehemu takatifu ndo ya kulia chakula halali na kutendea matendo mema,ni pamoja na kufunga ndoa humo na Kufanya Ibadah pia huyo mdau naona labda katoka home siku nyingi na nchi anayoishi hakuna aina yoyote ya Ibdah si Kanisa wala Msikiti,na huyo mdau aliyesema kula chini wanakokanyaga na viatu yuko wrong hapo ni msikitini hairuhusiwe kuingia na viatu,sasa hao baktelia ni wapi tena,ni kama mtu uko kijijini kwenu hakuna meza ya chakula huwa wanatandika mkeka chini mnakula katika sahani moja au kujipakulia katika sahani yako,,na hata hivyo kwa kuwa ni sehemu ya kuswalia ndo maana imeanza karatasi ya plastic chini!!!1Huyo mdau alovaa kanzu na koti namfananisha na shemeji yangu wa hapo Upanga mume wa mdogo wangu Amina!Mwambie Amina Da yako wa Mtaa wa Lugalo Upanga anaeishi UK anakusalimia!Mbona napatwa na wasi wasi naona kama wewe ndo bwana harusi maana bwana hakutajwa na wewe umevalia kibwana harusi!!!!EEe isije kuwa umetuongezea mke wa pili,,uke wenza hatutaki!Ahlam UK,
ReplyDeleteAnkali naona unapeleka Kipunga....sasa na izo nyama nani aliibuka kidedea Mwisho wa siku..ungeendelea kutuonesha picha hadi mwisho wa hiyo mechi.
ReplyDelete