ankal akijumuika na wadau katika mpunga wa harusi msikiti wa Swahilina uliopo Kinondoni block 41 baada ya Swalat 'Jumaa
 Katika kupiga mpunga kuna mikao aina kwa aina
 Na waandaaji wanapochelewa hali huwa hivi....maana mikono ishaanza kukauka ati
Ewaaa... tonge nyama sasa. Biriani swaaaaafi kabisa hili..
bado ndizi tu na mfuko wa rambo. huto tukombe ni halua hiyo...ya dessert

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2011

    Mh! Haka kasahani katawatosha kweli? Halafu huo mkao wako unaonekana hujala mpunga muda mrefu. Hizi fiesta noma.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2011

    Anko huyo mkao wako matata sana , naona unavinya mpunga uku kidole kimoja kinapiga hatua karibu karibu na minofu hilipo! ahhahah hapo anasubiriwa mmoja tu ajidusu kugusa nyama .ahhaa
    mdau paris

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 23, 2011

    Karne hii bado kuna "zunguka mbuyu"? Michuzi umesahau ndizi na kifuko cha rambo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 23, 2011

    Hapo mjanja nani? Maana naona nyama ziko kati lakini mjanja kazisukumia kwake kiaina. Duuh Ankal mjanja wewe.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 23, 2011

    Mikono wananawa au? Kwa sababu naona wengine wanashika pua na mokono hiyo hiyo itaenda kwenye sahani? Salaaale.

    ReplyDelete
  6. Mmpunga huo unanikumbusha Maulidi ya nyumbani. Enjoy!

    ReplyDelete
  7. Jamaa linakula peku peku huku limevaa saa? Ustaarabu gani huu?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 23, 2011

    ulaji huu unatakiwa uzoefu hasa kwa wale tuliozoea vijiko ni kazi kwelikweli.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 23, 2011

    piga mpunga macho kwenye nyama hahaha ankali kumbe ushakula chumvi nyingi nakuona yasmini zimeanza kuchanua kichwani hahaha

    hivi ankali muda mwingi unakuwa kwenye minuso ya nje hivi shangazi yangu unamuacha apike alafu huonekani unakula kona

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 23, 2011

    Baabuu naona umepiga koti iko ficha nini dani yake?
    pili pili che? ndiji che? yote dani ya koti. fuko nayo upoo?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 23, 2011

    Ankali Ndizi iko wapi??

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 23, 2011

    Mbona hukutuhabarisha vizuri, nani aliyeowa au kuolewa? Huyo mdau aliyevaa t-shirt anaonyesha msikiti anaujua siku za mpunga tu. Kumbe Ramadhani tayari, ndio maana harusi nyingi siku hiza!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 23, 2011

    Huyo jamaa aliyevaa saa inaonekana ni moto wa kuotea mbali na aliwapeleka kisawasawa.
    Ankal hivi kweli ni ustaarabu kulia ndani ya nyumba ya mungu? Mimi ni mkirsto,nauliza tu kwa sababu sikutegemea kitu kama hiki,watu mle humo humo then mnasalia humo humo,muogopeni mungu.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 23, 2011

    Inaelekea uliupania huo mpunga kuliko unavyopania kuangalia mechi za bwawa la ndubwi.......

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 23, 2011

    kwa kweli,twende mbele na turudi nyuma. Haina maana kwakua babu zetu walikaa chini wakila na sisi tufanye hivyo hivyo..huwezi kukanyaga hapo na viatu alafu ukaweka sahani hapo. Mikoni inapita sehemu nyingi kweli na hasa kwa joto tulilonalo na bakteria wengi, kwa nini vijiko havitumiki? kama ni watu wengi ni kweli tunahitaji kulia kwenye sinia lakini mikono mingi ni vizuri kutumia vijiko kupunguza kontakt na mikono ya wengine ambayo hujui kama imeoshwa vizuri.Mkao,inawezaje kula mbele ya wenzako na miguu iko juu? Ningependa tujiulize kidogo..chakula kinaitaji heshima and usafi..

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 23, 2011

    Aucle safi sana peleke ze ubwabwa!!huyu mshikaji anaeuliza kuuhusu kula msikitini mbona hata sie kanisanitwala sana tu?kwani hapo umeona kuna vileo?Mi ni mlutheri na makanisa yote tunaliamo labda hilo lako la kakobe ndo lina masharti kibao

    Mdau Manchester!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 23, 2011

    Mijitu mengine bwana Yesu kristo alikuwa anagawa mikate kwa vipande tugawane makanisani sasa leo unauliza kula kanisani? wewe vipi umesikia Chakula kwani kichafu?

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 23, 2011

    Kula msikitini kwani kuna ubaya gani jamani,kuna watu hawana makazi nchi za kiarabu kama wasafiri wanakaa msikitini kula chakula ni jambo la Kheri sana wala sio kilevi,na kanisani mbona watu huwa wanalishwa mkate,sehemu takatifu ndo ya kulia chakula halali na kutendea matendo mema,ni pamoja na kufunga ndoa humo na Kufanya Ibadah pia huyo mdau naona labda katoka home siku nyingi na nchi anayoishi hakuna aina yoyote ya Ibdah si Kanisa wala Msikiti,na huyo mdau aliyesema kula chini wanakokanyaga na viatu yuko wrong hapo ni msikitini hairuhusiwe kuingia na viatu,sasa hao baktelia ni wapi tena,ni kama mtu uko kijijini kwenu hakuna meza ya chakula huwa wanatandika mkeka chini mnakula katika sahani moja au kujipakulia katika sahani yako,,na hata hivyo kwa kuwa ni sehemu ya kuswalia ndo maana imeanza karatasi ya plastic chini!!!1Huyo mdau alovaa kanzu na koti namfananisha na shemeji yangu wa hapo Upanga mume wa mdogo wangu Amina!Mwambie Amina Da yako wa Mtaa wa Lugalo Upanga anaeishi UK anakusalimia!Mbona napatwa na wasi wasi naona kama wewe ndo bwana harusi maana bwana hakutajwa na wewe umevalia kibwana harusi!!!!EEe isije kuwa umetuongezea mke wa pili,,uke wenza hatutaki!Ahlam UK,

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 23, 2011

    Ankali naona unapeleka Kipunga....sasa na izo nyama nani aliibuka kidedea Mwisho wa siku..ungeendelea kutuonesha picha hadi mwisho wa hiyo mechi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...