Kaka pole kwa kazi, leo nilitaka kujua nahitaji nini ili niweze kupata Passport Book. Nilijua kwenye ukurasa wa wizara ya mambo ya ndani nitapata majibu, kwli nimepata majibu ila bado nina maswali yaliyokusa majibu. Ninaamini humu kwenye blog ya jamii nitapata majibu kutoka kwa wadau wenye uzoefu na baadaye wanaweza kunishauri mimi na hata wizara husika.
Ninayo yaandika na kuulizia yanatoka kwenye kiungo /link hii:
http://www.moha.go.tz/index. php?option=com_content&view= article&id=29&Itemid=135
1. Hapa chini (kwenye kichwa cha habari) kuna neno “PEROSNS” kwa kweli nimeshindwa kupata tafsiri yake, naomba nisaidiwe.
2. Ni kipi ninachotakiwa kikipata kwanza kati ya Passport Book na Tiketi (hasa ya ndege), maana hapa chini kwenye “OTHER SPECIFIC REQUIREMENTS BASED….” naona Tiketi ya kurudi / Return Ticket (kama sijakosea tafsiri) inahitajika.
USHAURI /MTAZAMO
Huu ukurasa wa wizara ya mambo ya ndani ni vema ukaandikwa kwa kiswahili harafu wahitaji /wasomaji wautafsiri kwa lugha yake kama ni kichina, kijerumani, kijapani n.k kuliko kuandika kwa lugha isiyo yetu na kukosea kosea.
PEROSNS ENTITLED TO PASSPORT OR TRAVEL DOCUMENTS
· An ordinary passport may be issued to any citizen of the United Republic of Tanzania for a purpose of travelling to outside the United ………
PROCEDURES FOR APPLICATION AND ISSUANCE OF NEW PASSPORTS.
Application for a new passport is……………………………………..
DOCUMENTS TO BE SUBMITTED TO SUPPORT APPLICATION FOR A NEW PASSPORT
Any application for a passport shall be accompanied by:
· A birth certificate or an affidavit of birth or certificate …………..
OTHER SPECIFIC REQUIREMENTS BASED ON THE NATURE OF THE TRIP ARE AS INDICATED HEREUNDER:
1. PRIVATE TRIP
The application for private trip shall be accompanied by:
· Proof of applicant’s activities
· Invitation letter
· Return ticket
Permission letter from the parent or …………………
Ni hayo tu kwa leo aksante.


Sasa ndugu mbona majibu yote unayo hapo juu sidhani kama unahitaji kingine zaidi ya kuwa na cha juu hicho ndo kitarahisicha kila kitu. Uhitaji kingine tena ndugu.
ReplyDeleteNdugu yangu katika suala la pasipoti kikubwa unahitaji kuthibitisha uraia wako kama mtanzania. Hili linafanyika kwa kuwa na chati chako cha kuzaliwa au kiapo cha kuzaliwa kama umezaliwa enzi hizo na ktk sehemu ambapo ni vigumu kupata cheti na cheti au kiapo cha mmoja wa wazazi wako. Pili unatakiwa kutaja madhumuni ya safari, hili ukiliangalia kwa undani utaliona halina maana lakini ni muhimu kwani kuna watu huwa wanatoroka au wanaenda kufanya biashara haramu nje ya nchi. Sio rahisi kumtambua mtu wa hivyo ila kama taratibu na kama utakamilisha basi ni vyema kwa afisa anayekuhudumia kwani likitokea lolote atakuwa na uthibitisho kwamba dhumuni la safari halikuwa baya. Sema taratibu zinatakiwa kuwa updated kutokana na wakati, zilizopo ni tangu enzi za mwalimu. watanzania wenye pasipoti nadhani hawafiki laki 5 kati ya watanzania wote millioni 40, inaonesha hatusafiri kabisa kuiona dunia. Huo ndio mchango wangu
ReplyDeletekwani ndugu google translator inafanya kazi gani au ndy kila kitu japo solution yake ipo tumia akili yako sipende mteremko.
ReplyDeletehuyo mtu anachodai pia kwamba yeye ni mtanzania na lugha aliyoisoma mpaka wakati huu anayoijua kiufasaha sio kiingereza anaomba hiyo fomu ya kuombea pasipoti ya tanzania iwe na lugha fasaha ya kiswahili ndiyo lugha anayoiweza kuisoma vizuri na kuielewa vizuri jamani serikali ya kibabe bado haijasema lugha ya taifa ni ipi maana hata wabunge wetu wanapokuja kuomba kura kwa walala hoi huzungumza kiswahili kizuri kabisa wakishaingia katika ukumbi wa bunge tu lugha inabadilika na inakuwa kiingereza je?hao waliokupa kura ili uwatete huko bungeni wanafahamu hicho kiingereza mnacho zungumza huko bungeni?au kunyanyasana au bunge kwa wageni tu sio wapiga kura wenu?mnafahamu vizuri wapiga kura wenu wangapi?au wananchi wenu wangapi?wanaofahamu lugha ya kiingereza?TAFADHALINI huo sio mwendo wa DEMOKRASI,na tuitukuze lugha yetu ya kiswahili kwa kila njia tusiwe malimbukeni,mdau bwegenaz.
ReplyDeleteBinafsi nilikuwa sijawahi kuupitia ukurasa huu wa idara ya uhamiaji Tanzania, lkn baada ya habari hii ndipo nikaupitia na nikagundua kuna haja ya maelezo ya kina,mfano mimi nina safari binafsi ya kimatembezi sasa nitapataje Ticket wakati sina pasipoti na huko kny ticket wanataka namba ya pasipoti? Nitakapokuwa nakata ticket nitajuaje tarehe ya kusafiri wakati sina pasipoti? Kwa Mchangiaji wa Sat Jul 23, 05:51:00 AM 2011 huyu bwana aliyetoa mada hii ana hoja ya msingi sema ameshindwa kujieleza.
ReplyDeleteHiyo inaitwa typo. Lakini pia sikuhizi huwezi kuuziwa tiketi kama huna VIZA. Pia huwezi kupata VIZA kama huna pasi! Kuku na yai!
ReplyDeleteWatu wengine bwana!!...Sioni hata cha kusaidia hapo, jaribu kuuliza jamaa zako mtaani pia kabla hujatoa vitu km hivyo kwenye Globu ya jamii..au unatafuta umaarufu tu!..mweeeeh!
ReplyDeleteRETURN TICKET MAANA YAKE NI TIKETI YA KWENDA NA KURUDI, NENDA SHULE UKASOME ENGLISH TENA KAKA OK!
ReplyDelete