Kijana Pascal Issa mkazi wa Tegeta jijini Dar es Salaam ameomba msaada wa fedha au matibabu kwa ajili ya upasuaji wa mguu wake wa kulia wenye mifupa miwili, Kijana huyo aliyefika katika Ofisi za MO BLOG jijini Dar es Salaam.

Aidha Kijana huyo amewaomba wasamaria wema kumsaidia ili aondokane na mateso anayoyapata hususani wakati wa usiku ambapo mfupa huo wa ziada ulioanza kujitokeza tangu akiwa na umri miaka 7 mpaka sasa akiwa na miaka 24 kuendelea kukua bila matumaini ya kupata matibabu.

Kwa yoyote atakayeguswa na tatizo la kijana huyo awasiliane naye kwa namba +255657069870 au awasiliane na Meneja wa MO BLOG kwa namba +255714940992 kwa ajili ya mawasiliano zaidi.

MO BLOG inawaomba wadau wanaoweza kumsaidia hata kupata Daktari wa kumtibu kwani kutoa ni moyo na hujafa hujaumbika.
Hii ni Sehemu inayoonyesha mfupa huo wa ziada unaoendelea kukua na kumsababishia maumivu makali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 02, 2011

    Zile pesa za posho za waheshimiwa wabunge singeweza kusaidia matibabu kama haya.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 03, 2011

    Ushauri wa bure kwa MO Dewji, Hizi taarifa zikikufikia uwe unazimaliza juu kwa juu... kila mtu nchi nzima anajua utajiri ulionao... Unasaidia Simba na Mpira wa Tanzania yatakushinda haya ya surgery moja mbili za hapa na pale??? Au kama vipi toa zile posho wanapigia kelele chadema bungeni zitumike kwa kijana huyu Tafadhali...


    Hebu waheshimiwa Wabunge na Mawaziri Acheni Ubinafsi na muangalie mambo kama haya ya msingi jamani, na nyie mtakufa kama sisi walalahoi, sasa sijui hizo mali zenu mnazojilimbikizia mtaenda nazo Kaburini au La...Waziri Mkuu alisema eti posho ziendelee kwakuwa wanaenda watu bungeni kuwapiga mizinga ndio zinaishia hapo hapo... Lo, Mzee mzima Hana Haya??

    Michuzi, Hata Ukibania, Ujumbe utakuwa umekufikia wewe binafsi na timu yako....Muogopeni Mungu jamani, Kesho mtaondoka kama walivyoondoka waliotangulia...

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 03, 2011

    Ni kweli kabisa!

    Naamini kwamba Mh.Mo alipofikisha ombi hili alitegemea wadau kutoa misaada ikiwemo ya mawazo na fedha. Khy maoni kuhusu matumizi ya POSHO wanazopata wabunge zingeweza kutumika kutatua tatizo la Pascal Issa na wengine wenye shida pia.

    Hivyo Mh. Mo ni vema akayapa mawazo haya uzito na kulifahamisha bunge kilio cha wananchi na namna fedha za posho zinavyoweza kusaidia wananchi kama Pascal Issa. hii ndio namna ya kupata maoni ya wananchi kutatua mattz ya wananchi kwa faida ya Taifa zima.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...