Gari hili lenye nambari za usajili T 893 AQR aina ya Nissan Sunny limegonga mtu asubuhi hii na kumsababishia kifo katika maeneo ya Jangwani,Mtu huyo ambaye jina lake halikuweza fahamika mara moja amepoteza maisha kutokana na kugongwa na gari hiyo wakati akivuka barabara ya Morogoro.Dereva wa gari hilo baada ya kusababisha ajali hiyo alitoweka na mpaka sasa hajulikani alipo na kuliacha gari hilo barabarani.
 Sehemu ya Gari iliyoumia kutokana na Kumgonga mtu huyo.
 Break Down iliyokuwa ikipita njia maeneo hayo ilibidi isaidie kuitoa gari hili barabarani na kuliweka kando maana lilikuwa likisababisha msongamano wa magari mengine.
 Wakazi wa maeneo ya jirani na eneo la tukio wakiwa wamejitokeza kwa wingi kuangalia mwili wa marehemu huyo ili kuona kama wataweza kumtambua.(KUMRADHI: hakujaweza kuweka picha ya marehemu huyo kutokana na kuharibika vibaya sana usoni)
Wanausalama Barabarani wakijadiliana namna ya kuweza kuubeba mwili huo na kuupeleka mochwari ili taratibu zingine ziweze kufuatwa.hivyo kama ukiona kuna ndugu yako humuoni nyumbani basi nenda hospitali ya Muhimbili kumuulizia maana mpaka tunaingia mitamboni,jina la marehemu lilikuwa bado halijatambulika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...