Gari hii aina ya Nissan Blueburd yenye nambari za usajili T 788 APB imegongana na lori la kubeba mchanga aina ya Isuzu lenye nambari za usajili T 930 BNT maeneo ya Victoria,barabara ya Bagamoyo rodi jijini Dar usiku huu.kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo,wanasema kwamba waliiona gari hii ndogo ikitokea upande wa mwenge na kueleke upande wa morocco huku ikiwa katika njia ya katikati iliopo katika barabara hiyo huku upande wa morocco kuelekea upande wa mwenge kulikuwa na hilo lori ambalo lilikuwa likielekea upande huo na baada ya kuiona gari hiyo ndogo ikizidi kuelekea wake ndipo dereva wa lori hilo akipojitahidi kuikwepa gari hiyo ndogo bila mafanikio na mpaka kupelekea kutokea kwa ajali hiyo.Dereva wa gari hii ndogo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja,alikimbizwa hospitali kwa matibabu kwani alikuwa kavunjika mkono wa kulia pamoja na mguu.
Baada ya muda kidogo ilikuja BreakDown na kuibeba gari hiyo ndogo ambayo imeumia vibaya sana.
Muonekano wa nyuma wa gari hiyo.
Hii ndio lori iliyogongana na gari hilo dogo usiku huu.
Inaonekana kuwa dereva wa gari dogo hakuwa na uzoefu wa kuendesha usiku.
ReplyDeleteKWA KWELI INASIKITISHA; NA MUNGU ALIYE MWEMA AMEEPUSHA JANGA LA MAUTI HAPA. ILA WATANZANIA INABIDI TUJIFUNZE KUFUATA SHERIA MUHIMU ZA BARABARANI;;HATA ZILE ZA MSINGI TU; NA SI KWAMBA MWENYE GARI KUBWA NDIYE MBABE BARABARANI; AU MWENYE HARAKA NDIYE MWENYE HAKI BARABARANI.
ReplyDeleteHIYO BARABARA YA BAGAMOYO;TOKA MWENGE KWENDA MJINI INA HATARI SANA;MAANA KILA DEREVA ANAYEKAA LANE YA KATIKATI ANAJIONA ANA HAKI; HATA KAMA MSHALE UNAONYESHA KWAMBA MAGARI YANAYOTAKIWA KUWEPO KWENYE HIYO LANE NI YALE YANAYOELEKEA MJINI.HII MARA NYINGI SANA INATOKEA.NA BAYA ZAIDI UNAKUTA MAGARI YANAYOTOKA PANDE ZOTE MBILI YAPO KWENYE MWENDO KASI.MIMI BINAFSI SIKU HIZI NAIEPUKA SANA HIYO LANE YA KATI; MAANA WATU HAWAJUI SHERIA.
KUTAKUWA NA AJALI NYINGI TU ZA NAMNA HII KAMA MAMLAKA HUSIKA HAZITAINGILIA KATI NA KUONYESHA MAKALI YAO KATIKA UFUATAJI SHERIA.
HII ILIKUWA USIKU; MCHANA KWEUPEE;TRAFFIC WANAKAA HAPO KARIBU NA BREAKPOINT WANAANGALIA MAGARI YA KUKAMATA ILI WAPATE RUSHWA;LAKINI WALE WANAOVUNJA SHERIA WANAJIPITIA; WASIO NA HATIA WANATENGENEZEWA MAKOSA.
ASKARI WA USALAMA SIJAJUA KAZI ZAO BARABARANI BADO;ILIVYO SASA NI KUJIPATIA RIZIKI TU!