Wakongwe wa muziki wa dansi, Nasibu "Ras Nas"  Mwanukuzi (kulia) na Dekula "Vumbi" Kahanga wakiwasha moto mkali kwenye tamasha la Mela lililofanyika Oslo, Norway.  "Vumbi" mwenye makao yake Stockholm, Sweden, alipiga na bendi ya Ras Nas kama msanii mwalikwa. Tamasha la Mela mwaka huu limefanyika kwa siku moja badala ya siku nne kutokana na mauaji ya kinyama yaliyofanyika Oslo hivi karibuni. Shoo hii ya Mela ilihudhuriwa na umati wa watu takribani 40,000. Wasanii wengine waliokuwepo ni pamoja na Ky-Mani Marley, Maryam Mursal, Linton Kwesi Johnson na Sain Zahoor.
Madansa wa bendi ya Ras Nas wakifanya wakionyesha umahiri wao wa kucheza mbele ya umatu mkubwa uliofika kwenye tamasha la Mela lililofanyika Oslo,Sweden.
Shukrani kwa mashabiki ikitolwewa na wanamuzi Ras Nas na Dekula Kuhanga pamoja na wanamuziki wengine.
Nyomi la Maana lililojitokeza kwenye shoo ya tamasha hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 30, 2011

    Hivi Sweden nako kuna Oslo? Mie nilidhani huo ni mji mkuu wa Norway.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...