Wakongwe wa muziki wa dansi, Nasibu "Ras Nas" Mwanukuzi (kulia) na Dekula "Vumbi" Kahanga wakiwasha moto mkali kwenye tamasha la Mela lililofanyika Oslo, Norway. "Vumbi" mwenye makao yake Stockholm, Sweden, alipiga na bendi ya Ras Nas kama msanii mwalikwa. Tamasha la Mela mwaka huu limefanyika kwa siku moja badala ya siku nne kutokana na mauaji ya kinyama yaliyofanyika Oslo hivi karibuni. Shoo hii ya Mela ilihudhuriwa na umati wa watu takribani 40,000. Wasanii wengine waliokuwepo ni pamoja na Ky-Mani Marley, Maryam Mursal, Linton Kwesi Johnson na Sain Zahoor.
Madansa wa bendi ya Ras Nas wakifanya wakionyesha umahiri wao wa kucheza mbele ya umatu mkubwa uliofika kwenye tamasha la Mela lililofanyika Oslo,Sweden.
Shukrani kwa mashabiki ikitolwewa na wanamuzi Ras Nas na Dekula Kuhanga pamoja na wanamuziki wengine.
Nyomi la Maana lililojitokeza kwenye shoo ya tamasha hilo.
Hivi Sweden nako kuna Oslo? Mie nilidhani huo ni mji mkuu wa Norway.
ReplyDelete