Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 23 (U23) itacheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa dhidi ya timu ya Taifa ya Shelisheli kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha. Kiingilio cha chini katika mechi hizo kitakuwa sh. 3,000.

Kwa jukwaa kuu kiingilio kitakuwa sh. 10,000 wakati kiingilio kingine ni sh. 5,000. Timu ya Shelisheli tayari iko jijini Arusha ambapo iliwasili Julai 22 mwaka huu mchana ikitokea Nairobi, Kenya tayari kwa mechi hizo.

Mechi ya kwanza itachezwa Julai 27 mwaka huu, wakati nyingine itakuwa Julai 29 mwaka huu. Mechi zitaanza saa 10 jioni, na Shelisheli inatarajia kuondoka nchini kurejea kwao Julai 30 mwaka huu kwa kupitia Nairobi.

U23 ambayo iko chini ya kocha Jamhuri Kihwelo imeondoka leo asubuhi (Julai 25 mwaka huu) kwenda Arusha. Itafanya mazoezi yake ya kwanza jijini humo leo jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Kaluta.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen pia yuko na timu hiyo akitoa ushauri wa kiufundi baada ya kuongeza wachezaji Haruna Moshi ‘Boban’ wa Simba, Juma Seif Kijiko wa Yanga na mfungaji bora wa michuano ya Kili Taifa Cup, Gaudence Mwaikimba wa Moro United kwa lengo la kuangalia viwango vyao kwenye mechi hizo ili kuona kama watamfaa kwenye kikosi cha Stars.

Baada ya mechi hizo, Julai 30 mwaka huu jijini Arusha, Poulsen atataja kikosi cha Stars ambacho kitaingia kambini Agosti 2 mwaka huu kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Palestina.

Taifa Stars inatarajia kuondoka Agosti 7 mwaka huu kwenda Palestina kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Agosti 10 mwaka huu jijini Ramallah. Timu itarejea Agosti 11 mwaka huu.
 
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...