wachezaji wa red Sea wakimzonga Refa kwa madai kuwa anawauma hasa baada ya refa kuwataka Yanga kurudia penati baada ya kukosa - mara mbili

Beki wa Red Sea akiokoa mpira huku Davies Mwape akiukodolea macho


 KIPA WA YANGA AKIOKOA PENAT I YA MWISHO
 askari wakiweka ulinzi kwa waamuzi wa leo


Mashabiki wa Yanga wakifurahia ushindi

 Mshambuliaji wa Yanga, Davies Mwape akitafuta mbinu za kuwatoka walinzi wa Red Sea katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya kombe la kagame kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam. Yanga ilishinda bao 6-5 za matuta baada ya kumaliza dakika 90 bila kwa bila. Katika penati tano-tano timu zote zilikosa penati moja moja kabla ya Yanga kushinda kwa penati yan mwisho iliyopigwa na Nurdin Bakari
Mshambuliaji wa Yanga, Kigi Makasi akimtoka beki wa Red Sea, Yakob Tekie katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya kombe la kagame kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam. Picha zote na Francis Dande wa Globu ya Jamii 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 06, 2011

    Wewe mithupu embu malizia kabisa kwa kusema "Ushindi wa Mbeleko".... Yaani kiwango cha Yanga ni cha chini mno... Kazi kubwa inahitajika kufanyika

    ReplyDelete
  2. Yanga wamerudia kupiga Penati mara mbili baada ya kukosa!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 06, 2011

    CECAFA and TFF tunajua wanawabeba simba na yanga ili wachezaji final, na wanachotafuta wao ni fedha pumbavu. Team mbovu mnazibeba for what??? ndio maana East africa teams viwango ni vibovu, michuano ya CUF hatuambulia kitu pumbavu kabisaa

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 07, 2011

    Kwa style hii ya hawa marefa kufanya upendeleo wa wazi wazi hivi ndio maana mpira wetu hauwezi kwenda mbele. Bingwa wa kweli hawezi kupatikana ktk mazingira kama haya. Ni aibu tupu, tunalipa viingilio vikubwa tuone mpira wa kweli badala yake marefa wanaonesha madudu ya wazi.

    Kwa sheria za soka kama kipa akitoka mapema na akaiokoa, pigo linarudiwa lakini ukapaisha mpira juu penalty hairudiwi. Hili lipo wazi, cha ajabu refa aliamuru pigo lingine wkt mpira ulipaishwa...!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 08, 2011

    Nasikitika sana kwanini penalti ya KIGI MAKASI haikurudiwa wakati gilikipa alitoka mita mbili wazi. Huu ni upuuuzi wa marefa kuogopa kufanya maamuzi magumu kisa tu wamesharudia mara mbili. Golikipa wao hajafundishwa kudaka penalty halafu mashabiki wa simba masikini weee, hawajui sheria za soka. Wanajua sheria za rufaa tu.....

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 09, 2011

    HIVI KWA STAILI HII YA KUZIBEBA SIMBA NA YANGA MNAONA SOKA LETU LITAKUWA KWELI? TIZAMENI WEZENTU WANAJUA MPIRA NA WANAJUA NINI WANAKIFANYA WAWAPO UWANJANI, TFF MNAJUA ULAJI TU POLENI SANA

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 09, 2011

    TANZANIA BWANA MNACHAKACHUA MPAKA KWENYE MPIRA JAMANI?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 09, 2011

    TFF MNATIZAMA MASLAHI TU NDIO MANA KILA SIKU TUNAKUWA VICHWA VYA WENDA WAZIMA (TANZANIA MTASHUKA KIWANGO MPAKA MTAFIKIA 0)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...