Bendi Maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya The Ngoma Africa Band aka FFU ughaibuni (pichani) watapiga kwata katika gwaride la wazi mjini Aschweiler, nchini Ujerumani siku ya jumamosi 20.08.2011 kuanzia saa 12.00 jioni.
Maporomota wa muziki huko ughaibuni wameamua kuifanyia kweli bendi hiyo maarufu kwa kuipangia ratiba ya maonyesho bila kupumua !
Kamanda Ras Makunja na kikosi kazi chake Ngoma Africa band aka FFU wamejikuta wapo katika kibarua sugu cha kuwapa burudani kamili wapenzi wa muziki katika kila kona huko ughaibuni.
FFU kw sasa wanatamba na nyimbo mbili mpya "Bongo Tambarare " na "Supu ya Mawe" wasikilize mwenyewe @ www.ngoma-africa.com


ffu gwaride lenu linakubalika,na vilio vyenu watoto wa mbwa vinasikika
ReplyDeletekwa ukali,kazenu mikanda