Kijana aliyeripotiwa kupotea, sasa amepatikana
Kijana huyo (pichani juu) alipatikana huko Vikindu katika wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani.

Kwa mujibu wa maelezo yake kijana huyo ambaye ana tatizo kidogo la akili alisema baada ya kutoka nyumbani alikokua anaishi (Chang’ombe Bora), alishindwa kujua njia ya kurudia hivyo akawa anaenda pasipo kujua anaenda wapi mpaka akaibukia huko Vikindu.Kijana huyo aliletwa na mama  msamaria mwema ambaye alimwona akirandaranda mitaani kwao.
Kwa mujibu wa maelezo yake kijana huyo baada ya kupotea alikua analala barazani  kwa watu na wakati mwingine analala kwenye matairi ya magari mabovu.Kula kwake nako ilikua ni kwa kuomba omba na wakati mwingine alikua analala na njaa

Kama familia tunapenda kuwashukuru wale wote waliotuombea na kutupa moyo kwa kipindi chote hiki ,vyombo vya habari kama televisheni, radio na blogs ambazo zilitoa tangazo la kupotea kwa kijana wetu huyu na hata kuweza kupatikana na kurudi tena nyumbani

Mungu awabariki sana sisi kama familia hatuna cha kuwalipa ila Mungu mpaji wa yote ndiye atakayewalipa
Kwa habari zaidi  gonga hapa   http://www.kichila.blogspot.com/
Ahsanteni sana

Mama Sabina Lujuo
(kwa niaba ya familia)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Poleni sana wanafamilia kwa hili.
    Tunashukuru Mungu kuwa kijana hakudhulika. Ninashauri kuwa serikali au mjasilimali fulani atengeneze vitambulisho ambavyo watu wasiojiweza wanaweza kuvaa kama kidani ( Dog Tags) hivi shingoni kueleza majina yao na namba ya simu ya kupigwa iwapo mtu yeyote anaweza kumuona mgonjwa. HIi itasaidia hata wazee wenye kiharusi, nao huwa wanapotea sana.
    Mungu aendelee kuwabariki kwa hili na mengineyo katika kumsaidia kijana aishi maisha yenye tija.

    ReplyDelete
  2. Jamaniinasikitisha na kufurahisha kuwa kijana kapatikana masikini kijana bado mdogo na kijana mzuri jamani,,,Alhamdulillahi hakuzulika kama usemavyomdau hapo juu na ni kweli kufaa alama ya maandshi ya kukutambulisha wewe na simu ni muhimu mno kwani kuna watu wengine masikini huwa wanashukiwa wizi na wanapigwa bure saa nyingine mpaka kufa kisha baadae ndo inakuja kujulikana kama mtu huyo ni mgonjwa au alikuwa tu kapotea,,,kweli serikai ya Tz inahitaji vitambulisho maana sasa hata watu wageni wamekuwa wengi mno TZ mpaka tabia ya waTZ ilikuwa nzuri inaanza kutoweka kwa kuwa wageni wengine majirani kama wakenya waganda warundi n.k wametuchangia changia vitabia kwa hiyo wengine watanzania wamekuwa wezi wakatili na mambo mengine mabaya tu ambayo tulikuwa hatuna,,,,kwa hiyo nashauri sio kila mtu apewe kitambulisho ni mpaka nzawa tu wa TZ!Poleni na Ongereni wana Familia,,,muwe waangalifu kwa huyo kijana!Mbalikiwe mno!Ahlam UK!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...