Leo natimiza miaka sitini tangu kuzaliwa. Huu si umri mdogo, nami namshukuru Muumba kwa kunipa fursa ya kuwepo ulimwenguni kiasi hiki. Ninavyokumbuka maisha yangu, ninatamani kama ningekuwa nimefanya mengi na makubwa zaidi kuliko niliyofanya kwa manufaa ya wanadamu. Ninatamani kama ningekuwa nimejiepusha na mabaya, nikawa mtu bora wa kupigiwa mfano. Lakini haiwezekani tena kuirudisha miaka iliyopita. Bora niangalie mbele, nijaribu kufanya bidii zaidi, ingawa sijui nimebakiza miaka mingapi hapa duniani.
Kumtembelea Prof Mbele BOFYA HAPA
Kumtembelea Prof Mbele BOFYA HAPA



Hongera profesa kwa kutimiza miaka 60, tunatazamia umefanya uvumbuzi wa kutuletea maendeleo katika nchi yetu!!
ReplyDelete